Home DOKUMENTARI Zlatan ambwatukia Mourinho

Zlatan ambwatukia Mourinho

12051
0

sehemu ya 8

Hii ni historia ya maisha ya mchezaji wa Zamani wa Man United na timu ya taifa ya Sweden Zlatan Sefik Ibrahimovic;

ilipoishia: Amini usiamini hakuna dhuluma inayodumu. Unajua kwanini Zlatan alimvunja kwa makusudi Raphael Van Da Vaart pale Ajax? Basi Lucciano Moggi ndiye mhusika mkuu. Kivipi?

Privaldinho
Na Priva ABIUD
Nilikutana na Zlatan tukaongea kwa muda wa lisaa kule Montecarlo kwenye mashindano ya Formula One. Nikamuuliza kuhusu kujiunga naJuventus. Alilalamika kuwa Juventus ni kama gereza. Nikamwambia hapana.
Moggi: Ni kweli hata mimi hapo zamani nilidhani Juventus wachezaji wanabanwa sana. Lakini sio

Nilipofika hapa niliwaambia wachezaji kuwa waishi maisha wayatakayo, kama ni kutafuta wapenzi/wanawake wafanye hivyo lakini katika maeneo sahihi sio kila mahali ambako wataonekana na watu ovyo ovyo.

mambo sio ndio haya sasa

Klabu ya Juventus haiwabani kabisa wachezaji kuishi maisha yao binafsi. kikubwa kila mchezaji ajiline kukwepa kashfa mbalimbali hasa kuhusu starehe za ovyo ambazo ziharibu taswira ya mchezaji na klabu kwa ujumla. Sisi Juventus tulimfuatilia mchezaji pale tu tulipopokea taarifa juu ya kuporomoka kwa kiwango chake. Zlatan alinielewa lakini akaniambia kuwa haoni mwanya wa yeye kuondoka Ajax. Nilimuuliza shida ni nini? Akanijibu kuwa anategemewa sana.

Zlatan Kazi unayo Mzee baba.

Nikamwambia tengeneza ugomvi na makusudi na Van Da Vart hawatakuvumilia” hii ilikuwa nukuu ya Lucciano Moggi iliyopo kwenye ktabu chake cha Il Pallone Lo Porto Io. Moggi alikuwa Mkurugenzi mkuu wa La Vecchia Signora (Juventus).

Baada ya sakata la Juventus kushuka daraja Zlatan aliondoka zake na kwenda kujiunga katika klabu ya Inter Milan.

Maisha yake ndani ya Inter hayakukumbwa sana misukosuko kwani tayari alishwakuwa mchezaji mkubw anayeheshimika. Mwaka 2014 Mourinho aliingia kwenye mgogoro na Ibra, baada ya kugoma kumfanyia mabailiko. Zlatan alikasirishwa na kitendo cha wachezaji wa Inter kucheza kivivu na kutaka atolewe nje ya uwanja kuliko kuendelea kucheza na watu ambao hawajitumi.
Zlatan alimkimbilia Mourinho na kumwambia anataka kutoka.

Zlatan: Mourinho alijitolewa sana kwa ajili ya timu ndiyo maana hata mimi nilifanya hivyo hivyo. Nilikuwa tayari kuua kwa ajili ya Mourinho

“Sisi ni mabingwa, nimepigania mafanikio haya, kwanini hawataki kunisaidia mimi kuwa mfungaji bora”. Maneno ya Ibra kwa Mou.

Morinho alipoulizwa kuhusu tukio lile alisema “Ni kweli Zlatan alinifuata nje akiwa na hasira sana. Wakati ule alikuwa anapigania kiatu cha ufungaji bora. Aliponiita Nikajifanya sijamuelewa, nikamuuliza, nini? unasemaje? Sikusikii,

Aliponisogelea, mikajifanya nipo bize nawafokea wachezaji wengine nikamrushia maji wala hakuyachukua, nikamrushia tena maji mengine nikawa simsikilizi tena ila namsisitiza sana atulie atapata goli nikampiga mgongoni arudi uwanjani huku nikimpa motisha kwa kumfokea kama rafiki na kumpa malekezo ya uwongo na kweli.

Dakika chache baadae Zlatan alifunga goli zuri sana”. Ikumbukwe hapo awali Jose Mourinho mwaka 2008 Mourinho alisema kwamba “Ronaldo ni mchezaji mzuri sana, alistahili mpira wa dhahabu kwa kuwa klabu yake ilitwaa UEFA na ligi kuu lakini kwangu mchezaji aliyeonesha kiwango bora ni Ibra.

Mourinho na Ibra walikuwa marafiki wakubwa sana. Zlatan anasema siku ya kwanza kukutana, Mourinho alimfuata Helena (mpenzi wa Ibra) na kumwambia kuwa, “unajukumu moja tu, kumlisha Ibra, kuhakikisha amelala salama, na kuhakikisha ana furaha kila mara”

KIFURUSHI

Jina Helena Seger
Utaifa Sweden
Kuz. August 25, 1970

(Miaka 47)

Mah. Lindesberg,

Orebro County

Nyota Virgo
urefu 1.65 M
Baba Ingemar Seger
Mama Margareta Seger
Ndugu Henrik Seger

Karin Seger

Watoto Maximilian Ibrahimović,

Vincent Ibrahimović

Zlatan na Familia yake (Mkewe na watoto wao)


Nilifurahia sana maisha yangu na Mourinho tatizo tulidumu kwa mwaka mmoja tu. Mourinho alikuwa ananipigia simu kila mara. Hata tukifungwa alikuwa hamnunii mchezaji, ni mpambanaji sana. Yupo tofauti sana na Guardiola, Guardiola na mbaguzi mno. Hajali na ana matabaka.

Picha bora kabisa katika maisha ya soka ya hawa Jamaa watatu (Zlatan, Guardiola, Mourinho)

Mourinho pia alielezea suala la Zlatan kuondoka Inter.
“Mwishoni mwa msimu nilikwenda nyumbani kwa Ibra. Akaniambia kama ni masuala ya usajili sipo tayari kukusikiliza. Nahitaji kuondoka na kwenda kutafuta maisha mengine. Kwa kawaida yangu sipendi kumzuia mchezaji kuondoka. Hakuna mchezaji aliye juu yangu. Klabu sio mchezaji mmoja. Nilimweleza ukweli licha ya kwamba hakutaka kusikia.

Najua dhamira yake ni kubaki Inter ila kwa kuwa tayari magazeti yalishaandika habari za yeye kubadilishwa na Samweli Eto’o hakufurahishwa na kitendo kile.

Nilimwambia bodi ya Inter imekaa imeweka chaguzi mbili (hatuna mpango wa kukuuza, au uuzwe kwa kubadilishana na Eto’o pamoja na Hleb kwa mkopo pamoja na Euro million 50” Kisha Zlatan haelewi chochote yupo tayari kuondoka kwa njia yoyote. Mimi kama kocha sikuwa tayari kumpoteza Zlatan.
Lakini pia upande wa pili niliwaza sana kwa kina. Hasa kiasi kile cha pesa ni ngumu bodi kukataa, ilikuwa ni dili la Euro Milioni 100, na nilishashtukia nafsi ya Zlatan ilikuwa inawaza Barcelona. Kwangu mimi hakuna kitu Ibra ambacho amemzidi nacho sana Eto’o. Niliona wote ni wa kiwango sawa. Nilifahamu wazi Barcelona haimhitaji tena Eto’o kwasababu ambazo sikufahamu. Je kwanini nikatae dili kama hili? jioni yake nilipokea simu ya bosi.

unataka kujua kilichoendelea hadi Zlatan Kutimka? tukutane makala ijayo. makala hii imeandaliwa na Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here