Home Kimataifa ZE FAITA: Paul Labile Pogba kumbe ni Mkongo?

ZE FAITA: Paul Labile Pogba kumbe ni Mkongo?

4697
0

Siku kama ya leo amezaliwa fundi wa soka duniani, kiungo mwenye mbwembwe kuanzia nje na ndani ya uwanja, The World Cup Winner Paul Labile Pogba.

Pogba amezaliwa na mama Mkongo Yeo Moriba na baba yake ni raia wa Guinea marehemu mzee Fassou Antoine ambao walihamia Ufaransa mwaka 1992 ambapo miezi kadhaa tu baada ya kufika Ufaransa Pogboom alizaliwa?

Pogba alianza soka akiwa na miaka sita katika akademi ya US Roissy-en-Brien. Akiwa na miaka 16 mwaka 2000 alijiunga na Mashetani wekundu. Swahiba mkubwa wa Pogba kuanzia 2000 mpaka 2011 alikuwa Jesse Lingard pekee.


Alipoona hapati muda mwingi wa kucheza, Pogba aliomba kuuzwa. Akaelekea Juventus kabla ya kurudi kwa dau la £89 M. (Somo usishindane na wanaokudharau, fanya kazi yako kwa bidii ipo siku watakuja wenyewe)

Ukiachana na mama yale mzazi ambaye amekuwa msaada mkubwa, Pogba pia ana malkia wake wa nguvu ajulikanae kama Maria Salaues ambaye ni mwanamitindo raia ya Bolvia.

Pogba amekuwa msiri sana katika mahusiano yake. Mara ya mwisho Pogba kuonekana na mwanamitindo huyo ni mwaka 2017.
:
Hata hivyo mwaka 2018 mwanadada huyo alionekana akiwa amevaa pete ya uchumba alipokuwa amekaa na mama yake Pogba kule Luzhniki Urusi wakati wa kombe la dunia.

Hana mbwembwe sana kuweka hadharani maisha yake ya mahusiano

🏆🏆🏆🏆 Serie A
🏆🏆 Coppa Italia
🏆🏆 Supercoppa
🏆 Europa League
🏆 League Cup
🏆 World Cup

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here