Home Kimataifa “Zamalek wanatisha, lazima niombe msaada Misri” Hassan Oktay

“Zamalek wanatisha, lazima niombe msaada Misri” Hassan Oktay

4523
0

Kocha wa Gor Mahia Hassan Oktay amesima Zamalek ndio tishio kubwa kwao kuelekea michuano ya shirikisho.

Gor Mahia walifuzu hatua ya makundi baada ya kuwaondosha Nyassa Big Bullets, kabla ya kutolewa na Lobi Stars ya Nigeria kwa magoli ya ugenini.

“Kundi sio gumu sana lakini hawa Zamalek ni tatizo kwetu. Nitaongea na marafiki zangu wanaoishi Misri, na wale ambao wanafundisha timu kubwa wanipe mbinu ni kwa namna gani tutawaondosha” Hassan Oktay.

“Nitawatumia Wendo na Okeyo kuhakikisha waarabu hawafiki katika eneo letu. Tuna wakati mgumu kuziba pengo la Harun Shakava na Joash Onyango ambao wamesimamishwa na CAF” Oktay


KWINGINEKO

Nyota wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Nigeria Obi Mikel amerudi tena ligi kuu. Zamu hii ametua kunako klabu ya Muddleborough akitokea kunako klabu ya Tiajin Ted bure.

Obi alitumikia Chelsea kwa miaka 11 akashinda EPL-2, FA- 3, na klabu bingwa 2012. Obi Mikel ana miaka 31 tu na huenda akawa msaada kubwa wa timu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here