Home Kimataifa Zahera kuwa makini Yondani na Kindoki watakuponza

Zahera kuwa makini Yondani na Kindoki watakuponza

5022
0

Safari ya timu ya wananchi Dar es salam young Africans ya takribani mechi 19 pasipokupoteza Iliishia maeneo ya stand pale Shinyanga baada ya kupokea kichapo cha goli moja kwa bira toka kwa chama la wana Stand united goli la nahodha Jacob Massawe dakika za mwisho kabisa..
Baada ya siku tatu Yanga tena ikakubali kupokea kichapo kingine kwenye mashindano ya Sportpesa cup 2019 dhidi Kariobangs Sharks kwa jumla ya magoli matatu kwa mawili, pamoja na matokeo hayo Yanga walionekana kukosa nidhamu baada ya kufanya vitendo vilivyo kinyume na mchezo wa mpira wa miguu Kama kurusha ngumi na rafu nyingi zisizo na msingi

Tokea Kelvin Yondan avuliwe kitambaa cha unahodha ameonekana kufanya makosa mengi ya kiuchezaji na ya utovu wa nidhamu, amekua akitoa Pasi ambazo hazina macho kiasi kwamba kukaribisha mashambulizi huku kwa upande mwingine hakuna uwiano mzuri wa Yondani na Andrew vicent, heri pale Abdalah Shaibu na Yondani wakicheza pacha hufanya vizuri sana kuliko pacha ya Dante na Yondani.

Kindoki amekua akifanya makosa mengi sana hasa kwenye kufanya maamuzi ya kuwapanga mabeki na ye binafsi kwani mala nyingi hujikuta yuko nje na eneo husika(off target) na hafanya saves ambazo Kakolanya na Kabwili wamekua wakifanya.

Zahera Ana wajibu mkubwa sana kupunguza makosa ya Yondani na Kindoki pamoja na timu nzima kwa ujumla tofauti na hapo mechi zijazo Yanga watateseka sana Na kua na uwezekano mkubwa wa kupoteza zaidi.

Raphael Lucas(udom)
0710690782/0764764449

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here