Home Kitaifa Zahera ampa mbinu Ajibu kurudi Taifa Stars

Zahera ampa mbinu Ajibu kurudi Taifa Stars

3950
0

Mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa leo January 15, 2019 kati ya Yanga dhidi ya Mwadui, umemtambulisha rasmi Ibrahim Ajibu kama nahodha rasmi wa kikosi cha Yanga baada aliyekuwa nahodha Kelvin Yondani kunyang'anywa kitambaa cha unahodha kutokana na utovu wa nidhamu.

Katika mchezo huo, Ajibu amehusika katika mabao matatu ambayo Yanga imefunga dhidi ya Mwadui. Alianza kufunga bao la kwanza kwa free kick, akatoa pasi ya mwishi Tambwe akafunga kwa kichwa na alihusika katika goli la tatu ambalo lilifungwa na Feisal Salum.

Kocha wa Yanga Zahera Mwinyi amesema amekuwa akimsisitiza Ajibu na wachezaji wengine kuboresha viwango vyao ili waitwe timu ya taifa na endapo Taifa Stars itafuzu AFCON 2019 wawe kikosi.

“Nimemwambia Ajibu na wachezaji wengine kuwa Tanzania itafuzu AFCON, mtaifunga Uganda hapa, sasa hivi ndio wakati wa kumshawishi kocha wa timu ya taifa kwa sababu kuna miezi karibu mitatu kabla ya kucheza na Uganda ambapo mkishinda mtakwenda AFCON”-Zahera Mwinyi, kocha Yanga SC.

“Huu ndio wakati wa kumwonesha kocha wa timu ya taifa ili atakapotaja majina ya wachezaji kwa ajili ya mechi dhidi ya Uganda lazima ataangalia wachezaji wa timu inayoongoza ligi tangu mwanzo wa msimu hadi wakati huo hawezi kuwaacha.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here