Home Kitaifa Zahera aishauri TFF

Zahera aishauri TFF

3272
0

Kocha mkuu wa Yanga Zahera Mwinyi ametoa maoni kwa TFF kuangalia namna nzuri ya kuzisaidia timu zinazoshiriki michuano ya kimataifa.

Zahera amesema ratiba lazima iwe inatoa nafasi kwa timu inayoshiriki michuano ya kimataifa kwa sababu timu husika ikifanya vizuri ni faida kwa nchi.

“Viongozi wa TFF wanapaswa kuziangalia timu zinazocheza mashindano ya CAF na kuzisaidia zote bila kujali ni Simba, Yanga au Mtibwa.”

“Yanga tulienda kucheza Kenya na Gor Mahia siku mbili baadaye tukatakiwa tukacheze Shinyanga. Timu zisifanyiwe hivi ili kuwachosha wachezaji kwa makusudi kwa sababu Yanga ikifanya vizuri nchi inapata pointi nyingi na inaweza kuongezewa timu nyingine badala ya kutoa timu mbili zitakuwa tatu.”

“Sisi (DR Congo) tuna timu nne, Zambia wana timu nne kwa sababu gani Tanzania iendelee kubaki na timu mbili? Inabidi kuzisaidia timu zinazocheza mashindano ya CAF.”

“Walifanya vizuri kuipumzisha Simba kabla ya kwenda kucheza na Nkana ilikuwa vizuri, wachezaji walipumzika wakapata nguvu wakaenda kupata matokeo ya kufungwa 2-1 ambayo yalikuwa ni mazuri kwao.”

“Lakini haifai kuipumzisha Simba halafu ikifika zamu ya Yanga mnawaambia wacheze, mnakuwa mnapoteza wenyewe nafasi ya kuongeza timu kwenye mashindano ya Afrika.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here