Home Kimataifa Yule kijeba aliyekutana na Simba asaka klabu ya 20

Yule kijeba aliyekutana na Simba asaka klabu ya 20

4444
0

Hivi unawakumbuka wale Al Masry waliokuja kucheza na Simba mwaka jana? Sasa kuna jamaa wao yule kijeba pande la mtu miraba kama 7 hivi Aristide Bance.

Yule Bance mpaka sasa yupo pale pale Al Masry lakini inasemekana anataka kwenda klabu ya Horoya FC. Ikumbukwe mwaka jana alisema timu nyingi za waraabu hasa hasa ligi ya Misri inatisha kwa ubaguzi na kuwanyanyasa wachezaji weusi.

Bance alidai kuwa sababu kubwa wamisiri kufeli kombe la dunia ni kutokana na laana ya ubaguzi waliyo nayo kwenye ligi. Sababu hii imemfanya mchezaji asake timu ya kwenda msimu huu.

Bance ni mzaliwa wa Ivory Coast lakini ana uraia wa Burkina Faso kwa sasa. Bance ana undugu na yule nyota wa zamani wa Ivory Coast Aruna Dindane.

Rekodi kubwa ya huyu mwanaume ni kucheza vilabu vingi. Bance amecheza takribani vilabu 20 akiwa na umri wa miaka 34. Kwa sasa anasaka klabu ya 21. Na bado anasema anataka kucheza hata mpaka miaka 40.

Bance alianza kucheza soka la kulipwa 2000 katika klabu ya Stade d’Abbidjan. Ameichezea timu ya taifa ya Burkina Faco tokea 2003 michezo 73 na kufunga magoli 22. Tokea 2006 hakuwahi kuchezea timu kwa zaidi ya misimu miwili.

Wasifu
Msimu Klabu M G
2000 Stade d’Abidjan 33 (8)
2001 Athlétic Adjamé 30 (5)
2002 RFC Daoukro 20 (8)
2002–2003 Santos Burkina 16 (9)
2003–2006 Lokeren 77 (27)
2006–2008 Metalurh Donetsk 12 (2)
2007–2008 Germinal Beerschot (mkopo) 9 (0)
2008 Kickers Offenbach (mkopo) 10 (4)
2008–2010 1. FSV Mainz 05 62 (24)
2010–2012 Al-Ahli Dubai 7 (2)
2011 Umm-Salal (Mkopo) 8 (4)
2011 Samsunspor (Mkopo) 20 (5)
2012–2014 FC Augsburg 18 (0)
2013–2014 Fortuna Düsseldorf (mkopo) 10 (2)
2014 HJK Helsinki 4 (1)
2015 Irtysh Pavlodar 11 (2)
2015–2016 Chippa United 14 (3)
2016 Riga 8 (1)
2016–2017 ASEC Mimosas 26 (13)
2017–2018 Al-Masry

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here