Home Kitaifa Yanga, Singida, zapambania pointi mezani

Yanga, Singida, zapambania pointi mezani

3268
0

Uongozi wa Singida United umewasilisha malalamiko Bodi ya Ligi kupinga Yanga kumchezesha mshambuliaji wao chipukizi Gustava Simon (aliyevaa jezi namba 30) kwa madai kwamba amesajiliwa na Dar City ya ligi daraja la kwanza.

Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga amethibitisha kuwasilisha malalamiko Bodi ya Ligi.

“Tumewasilisha malalamiko yetu Bodi ya Ligi dhidi ya timu ya Yanga kwa sababu kwenye mchezo wetu wamemchezesha mchezaji ambaye kimsingi sio mchezaji wao halali anamilikiwa na Dar City na leseni yake ya uchezaji imetolewa kuichezea timu hiyo yenye makazi yake pale Ilala”-Festo Sanga, Mkurugebzi Singida United.

Yanga pia imewasilisha malalamiko ikipinga wachezaji Godfrey Mwashiuya pamoja na beki Zahir na kocha msaidizi Shadrack Nsajigwa kushiriki katika mchezo huo wakati waliadhibiwa na kamati ya saa 72.

Kuna ambao walitakiwa kukosa michezo mitatu pamoja na kulipa faini ya shilingi 500,000. Inaelezwa kwamba, wametumikia adhabu ya kutoshiriki mechi tatu lakini faini ya shilingi 500,000 hajalipwa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here