Home Kitaifa Yanga inaingia kama UNDERDOG

Yanga inaingia kama UNDERDOG

3927
0

Ukiangalia Simba kwa upande wa squad, mwendelezo wa matokeo lakini pia mazingira kuelekea kwenye mechi Simba wametoka kwenye mazingira ambayo inawezekana ikawa ni faida kwao au hasara.

Faida kwa maana ya kwamba wametoka kwenye hali ya ushindani kwenye mechi walizocheza za #CafChampionsLeague zilikuwa ngumu na mechi ya kesho ni ngumu vilevile kwa hiyo hawaendi kama wageni. Wametoka kukutana na timu zenye profile kubwa kama mechi wanayoenda kukutana nayo kesho.

Upande mwingine kucheza hizi mechi mfululizo zinaweza kuwa zimewasababishia uchovu lakini sioni kama ni tatizo kwao kutokana na kikosi walichonacho na ukamilifu wa wachezaji wote wa Simba.

Simba wanawachezaji zaidi ya 22 ambao wako vizuri kwa hiyo kocha anaweza kuamua kufanya mabadiliko kulingana na aina ya kikosi alichonacho.

Ukirudi kwenye kikosi cha Yanga, wamekuwa kwenye mazingira magumu hiyo inafahamika na mazingira hayo yamefanya wachezaji wengi kupata majeraha na kushindwa kuwa na consistency.

Kwenye eneo la kiungo (Tshishimbi, Buswita, Kamusoko) ni wachezaji muhimu lakini wamekuwa wanaingia na kutoka na wamekuwa hawana mwsndelezo mzuri ukilinganisha na upande mwingine. Mchezaji ambaye amekuwa na mwendelezo mzuri kwenye eneo la kiungo ni Feitoto.

Kwenye idara ya ushambuliaji, Makambo na Ajibu ndio wamekuwa wakipata nafasi mara kwa mara, Amis Tambwe anaingia na kutoka. Boban na Ngasa ni wachezaji ambao siwaoni kwenye level ya ushindani mkubwa ni wakongwe ambao wanasaidia kutengeneza umoja na kutumika kwa mpango maalum sio wachezaji wa kuwategemea 100% hasa kwenye aina ya mechi kama ya kesho.

Ukiangalia vikosi vyote na jinsi ambavyo timu zimekwenda, kwa mtazamo wangu Yanga inaingia kwenye mchezo wa kesho kama UNDERDOGS lakini Simba inapewa nafasi kubwa ya KUSHINDA.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here