Home Kimataifa Westbrook Na Durant Hakuna Tena Bifu.

Westbrook Na Durant Hakuna Tena Bifu.

3177
0
OAKLAND, CA - JANUARY 18: Kevin Durant #35 of the Golden State Warriors dribbles past Russell Westbrook #0 of the Oklahoma City Thunder at ORACLE Arena on January 18, 2017 in Oakland, California. NOTE TO USER: User expressly acknowledges and agrees that, by downloading and or using this photograph, User is consenting to the terms and conditions of the Getty Images License Agreement. (Photo by Ezra Shaw/Getty Images)

Inawezekana wengi wakawa walikuwa wanahisi ugomvi kati ya wachezaji marafiki wa zamani Russell Westbrook na Kevin Durant ungekuwa wa kudumu daima. Hii ilitokana na kitendo cha Kevin Durant kuamua kuondoka kunako klabu ya Oklahoma City Thunder pasipo kumtaarifu “mdogo wake” Russell Westbrook ambaye anadai aliona taarifa kupitia mitandao tu kuwa Durant alikuwa akijiunga na Golden State Warriors.

Hii ilipelekea watu hawa kuwa mahasimu kufikia hatua ya kwenye michezo inayowahusu kuonekana wakikwepana na kwenye moja ya michezo, Russell alionekana kumzuia mchezaji Ernes Kanter asisalimiane na Durant.

Lakini Kendrick Perkins ambaye alikuwa mchezaji wa Oklahoma City Thunder amesema aliwezesha wachezaji hawa kuweza kuzungumza tena japo kwa simu, na anasema mazungumzo hayo kati ya  Russell Westbrook na Kevin Durant yalifanyika siku ambayo Westbrook alivunja rekodi ya Oscar Robertson ya kuwa na Triple Double nyingi kwa msimu mmoja mwezi uliopita.

Perkins, ambaye alicheza na Westbrook na Durant katika klabu ya Oklahoma City Thunder kuanzia 2011 mpaka 2015, alizungumza kwenye kipindi cha  TNT’s “Area 21” ambacho ni cha Kevin Garnet.

Alisema kuwa aliamini hawakuwa na ugomvi mkubwa kiasi hicho bali ni watu tu na vyombo vya habari ndivyo vilivyokuwa vinapandisha ukubwa wa jambo hilo.

“Nahisi katika usiku ambao Russ alivunja rekodi, nilimtumia ujumbe Kevin Durant,” Perkins alisema, akiuzngumzia tukio la April 10, na hii ilikuwa kabla ya Westbrook na Durant hawajazungumza tangu Durant ajiunge na Golden State Warriors mwezi July.

“Siku iliyofuata tulikuwa tunazungumza kitu na akanitumia ujumbe akisema ‘mie na Russ tulikuwa na mazungumzo mazuri sana jana’ na vyombo vya habari havifahamu lolote kuhusu hili, lakini nimeamua tu kuwajulisha mfahamu alimaliza Perkins.

Perkins, 32, hajacheza kabisa msimu huu lakini pia ameweka wazi kuwa hajawa tayari kustaafu. Lakini pia ameongeza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa siku moja Durant kurejea katika klabu ya Oklahoma City Thunder.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here