Home Kitaifa Waziri Mkuu anataka taji la AFCON U17 libaki nyumbani

Waziri Mkuu anataka taji la AFCON U17 libaki nyumbani

2515
0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameliangiza hirikisho la soka nchini TFF lihakikishe Tanzania inaibuka na ushindi katika fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 mwaka 2019.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo asubuhi February 7, 2019 Bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto ambaye alitaka kufahamu, serikali inayahusishaje mashindano hayo ya AFCON na mkakati wa kuendeleza utalii nchini.

Waziri Mkuu amesema maandalizi yote yanaendelea kufanyika na serikali imejiandaa vya kutosha kupokea ugeni utakaowasili hapa ncbini.

“Tanzania kupitia serikali hii ya awamu ya tano imeridhia mashindano haya yafanyika hapa Tanzania na yanafanyika mwaka huu 2019.”

“Serikali imejiandaa kupokea wageni wote wanaokuja kushiriki mashindano yatakayofanyika nchi na serikali inaendelea na maandali hayo kwa kushawishi sekta zote zitakazonufaika na uwepo wa wageni hao.”

“Kupitia mashindano haya tumehamasisha mikoa ya jirani na maeneo ambako viwanja vitatumika, tumeambiwa viwanja vitatu vitatumika wakati wote wa mashindano. Maandalizi ya maeneo yote hayo yanaendelea kufanywa.”

“Niwahakikishie watanzania kuwa, ujio huu kwetu ni muhimu sana, tunatakiwa tushirikiane sote tuhakikishe tunapata mafanikio kutokana na wageni hawa kuingia kuishi hapa na kurudi kwao wakiwa salama.”

“Lakini pia shirikisho la soka Tanzania liendelee kuimarisha maandalizi ya timu yetu ambayo itashiriki kwenye mashindano haya ili hatimaye tuweze kuibuka kidedea.”

“Sisi sote watanzania tunawajibika kuonesha uzalendo kwa timu yetu ili kuitia moyo kwa hiyo mchango wa kila mmoja kwa namna yoyote ile unahitajika katika hili.”

“Niwahakikishie watanzania kuwa mashindano tumeyapokea tupo tayari kupokea na wageni wake na tutaendelea kushindana na timu ambayo itashindana naaminitutafanikiwa.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here