Home Kitaifa “Watu wanafikiri kuandaa timu ni sawa na kukata kachumbari”-Amri Kiemba

“Watu wanafikiri kuandaa timu ni sawa na kukata kachumbari”-Amri Kiemba

4905
0

Kitendo cha Azam kumtimua kocha Hans van Pluijm na msaidizi wake Juma Mwambusi wakiwa hawajamaliza hata msimu kimewashtusha wadau wengi wa soka.

Amri Kiemba akiwa kwenye #SportsRoundUp amesema kuna watu wanafikiri kuandaa timu ni rahisi na ni ishu ya muda mfupi unaanza kupata matokeo.

“Kuhusu performance ya timu na kuondoka kwa waalimu nafikiri watu wanadhani kuandaa timu ni sawa na kukata kachumbari yani ni kitu rahisi tu.”

“Ukiwauliza Simba wanajua hiyo kitu, wamechukua zaidi ya miaka minne nafasi yao nzuri ilikuwa ya tatu kwa sababu nao pia walidhani unaweza kuondoa watu ukaleta wapya timu ikaendelea kupata ushindi.”

“Kuna wakati viongozi huwa wanafikiri kwenye timu yao hata akienda nani timu itashinda tu. Azam waliifumua timu yao bila kujua itachukua muda mrefu wa kutengeneza timu ya kushindana kama iliyokuwepo.”

“Hans alikuwa anahitaji muda ili kuandaa timu, kwa timu aliyoikuta sikuwa natarajia msimu huu atapata mafanikio makubwa kwa sababu timu kama inatengenezwa upya kwa sababu kwa miaka mitatu iliyopita ukiangalia wachezaji walioipa Azam mafanikio utakutana na Aggrey Morris, Sure Boy na Domayo wengine wote wapya.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here