Home DOKUMENTARI Watoto wa magwiji wa zamani wa Ujerumani waliosaliti nyao za wazazi wao...

Watoto wa magwiji wa zamani wa Ujerumani waliosaliti nyao za wazazi wao wakutana

13703
0

Klabu ya Hertha BSC ilianzishwa mwaka  1892. Kwa sasa klabu hiyo wanacheza watoto wa miamba wa soka wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani. Watoto hao ni Pascal Kopke mtoto wa golikipa wa zamani waa faifa hilo Andries Kopke na mwingine ni mtoto wa Jurgen Klinsmann ajulikanae kama Jonathan Klinsmann.

Andries Kopke na Jurgen Klinsmann walikuwa wachezaji tegemezi kwa timu ya taifa ya Ujerumani.

Wazazi wao hawajakutana tu uwanjani kama wachezaji ila pia wamekutana kwenye benchi la ufundi la kuinoa timu ya taifa. Hapo awali Klinsmann akikuwa kocha mkuu wa Ujerumani kwenye michuano ya kombe la dunia na Kopke ni kocha wa makipa timu ya taifa tokea mwaka 2004 mpaka sasa.

Wasifu wa Jurgen Klinsmann
Majina Jürgen Klinsmann
Kuzali 30 Julai 1964 (54)
Mah Göppingen, Ujerumani
Kimo 1.81 m (5 ft 11 12 in)
Nafasi fowadi

Jurgen Klinsmann kama tunavyoona hapo juu yeye alikuwa fowadi matata sana wa timu ya taifa. Lakini hii ni tofauti kwa mwanae.

Wasifu wa Jonathan Klinsmann
Majina Jonathan Klinsmann
Kuzal April 8, 1997 (21)
Mah Munich, Germany
Kimo 1.92 m (6 ft 4 in)
Naf Kipa

Mtoto wake amefuata njia ya baba yake kucheza soka lakini hajafuata nyayo zake kucheza kama mshambuliaji yeye ameamua kuwa kipa.

Jonathan ana uraia wa mataifa mawili, Marekani na Ujerumani

Kwa Upande wa Andries Kopke

Wasifu wa Andries Kopke
Kuz 12 March 1962 (56)
Mah Kiel, West Germany
Kimo 1.82 m (6 ft 0 in)
Naf Kipa

 

Baba yake Pascal yeye alikuwa Kipa na aliichezea Ujerumani michezo 59. Kopke alipostaafu alitoa nafasi kuzaliwa golikipa mwingine bora katika ardhi ya Ujerumani Oliver Khan.

Alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Ujerumani mwaka 1993. Mwaka 1996 alipata mafanikio makubwa baada ya kubeba ubingwa wa Euro. Atakumbukwa vyema kwenye mchezo wa nusu fainali aliokoa mkwaju wa penati wa Gareth Southgate (Kocha wa sasa wa England) na kuiwezesha kufika fainali kabla ya kubeba taji hilo. Mwaka huu alichaguliwa kuwa kipa bora wa Fifa.

Mwanae Pascal yeye ameamua kwenda tofauti na baba yake. Yeye ameamua kucheza kama mshambuliaji na sio kipa. Kama ilivyo kwa Klinsmann mtoto wake kucheza nafasi tofauti na ya baba yake.

Wasifu wa Pascal Kopke
Kuz 3 Septemba 1995 ( 22)
Mah Hanau, Ujerumani
Kimo 1.75 m (5 ft 9 in)
Naf Fowadi

Kama tunavyoona hapo kuwa watoto hao wawili ambao kwa sasa wanacheza klabu moja ya Hertha hawajafuata nyayo za wazazi wao.

Watoto hao nyota hao kwa sasa wapo klabu moja lakini hawajabahatika kukutana timu ya taifa.

Klinsmann yeye ameichezea marekani kwenye ngazi ya vijana. Kwenye michuano ya 2017 CONCACAF U-20 Championship mtoto huyu wa Klinsman alitwaa tuzo ya kipa bora wa michuano.

Mtoto wa Kopke hajapata nafasi kubwa sana kucheza lakini aliwahi kuitwa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 lakini mpaka sasa hajafanikiwa kuitwa timu ya taifa.

DATA za Paschal Kopke 18/19

 M  G  G  D
2 1 90
1
1 1 90

Kwa bahati mbaya watoto hawajawahi kucheza pamoja. Ni mchezo mmoja tu ambapo wote walikuwa benchi dhidi ya Nuremberg. Kwa sasa Klinsmann yupo na klabu B.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here