Home Kitaifa Wataalam toka Ujerumani wamekuja kusaidia soka la vijana Tanzania

Wataalam toka Ujerumani wamekuja kusaidia soka la vijana Tanzania

2893
0

Kituo cha Magnet Youth Sports Organization kwa kushirikiana na Chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) wanaendelea na semina ya wiki moja iliyoanza jana kwenye viwanja vya JMK Park Kidongochekundu.

Semina hiyo ina lengo la kutoa elimu kwa walimu wa soka la vijana nchini namna ya kufundisha watoto. Semina inaendeshwa na wakufunzi kutoka Ujerumani (ITK).

Makamu Mwenyekiti wa soka la vijana DRFA Tuntufye Mwambusi ambaye pia ni mkufunzi wa kutoka kituo cha Magnet, anaeleza zaidi kuhusu ugeni huo na semina yenyewe.

“Program tunayoifanya inahusisha Magnet Youth Sports Organization na ITK kutoka Ujerumani ambao wanahusika na mambo ya International Sports kwa hiyo huwa kuna scholarships kutoka nchi mbalimbali duniani.”

“Hii project tunayoifanya tunahusisha pia mchezaji Yussuf Poulsen ambaye ni mchezaji wa timu ya taifa ya Denmark na klabu ya RB Leipzig ya Ujerumani kitu kizuri ni kwamba ana asili ya Tanzania baba yake alikuwa mtanzania nilipokuwa Ujerumani nilikutana nae tukaongea pamoja na chuo (Leipzig University) kuona namna gani tunaweza kusaidia Youth program za Tanzania.”

“Tukakubaliana tutafanya program ambayo italeta wataalam kutoka Ujerumani ili kuja kuwapa mafunzo makocha wetu wa Tanzania. Idadi ya makocha ambao wapo kwenye mafunzo haya ni 25 tutakuwa pia na watoto wapatao 120 kutoka kwenye academies mbalimbali za Dar es Salaam.”

“Tutatembelea pia shule tatu ili wenzetu waweze kuona sports inavyofanyika shuleni lakini pia watapata fursa ya kufundisha watoto.”

“Kupitia program hii tunategemea makocha watakaokuwa wamejifunza watapeleka mafunzo haya sehemu nyingine na yatakuwa na mchango mkubwa kwa sababu wanatoka kwenye academies mbalimbali.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here