Home Kimataifa Wasifu wa Emiliano Sala

Wasifu wa Emiliano Sala

3673
0

Wahenga wanasema, siku zote mtu sio mtu, mpaka akifariki ndo huwa mtu. Wengi tusinge mtazama, na dunia kwa ujumla isingeweza kufahamu uwepo wake. Lakini sasa dunia kote wanamjua. Na hakuna njia ya kufanya ili aweze kuhisi umaaruufu wake.Jina lake anaitwa Emiliano Raúl Sala Taffare. Alizaliwa tarehe 31 October 1990 hukoo Cululú, Santa Fe, nchini Argentina ambaye alikua ni mtoto wa dereva wa malori. Katika ukuaji wake Sala alikua anavutiwa na mchezaji nguli wa Argentina Gabriel Batistuta.Alikuwa akiangalia video za mchezaji huyo aliekipiga katika vilabu kama Fiorentina, As Roma na Inter Milan za nchini Italia. Uchezaji wa Emiliano ulianzia Ufaransa katika klabu ya Bordeaux akiwa na umri wa miaka 20 tuu.Baadae akapelekwa kwa mkopo Us Orléans na baadae tena Chamois Niortais za hapo hapo Ufaransa, baada kuonyesha uwezo mkubwa kocha mkuu wa Bordeaux akaamua kumrejesha katika kikosi cha kwanza , na mafanikio hapo Bordeaux hayakua mazuri kwani alikua na bao juu katika mechi 11 alizocheza, wakampeleka tena kwa mkopo SM Caen.Baadae alirejea Bordeaux. mwaka 2015 Emiliano alijiunga na klabu ya Nantes kwa mkataba wa miaka 5 kwa ada ya paundi €1 million. Kwa msimu huo alikua kinara wa klabuni hapo kwa idadi ya mabao 6, nakuwatamanisha vilabu vingi kimoja wapo ni Wolveampton wanderers ya uingereza, lakini Nantes wakawatema mbweha hao wanaowika nchini humo.Msimu uliofata Emiliano aliongeza ufanisi kwa kupachika mabao 12, na kuendeleza rekodi yake yakua mfungaji kinara wa klabu hiyo kwa mara tatu mfululizo. Mwanzo wa Msimu wa 2018-19 vilabu kama Galatasaray ya Uturuki vikavutiwa kuweka mzigo lakini suala la usajiri likashindikana.Na Emiliano akabakia Nantes na hapo alifanikiwa kuwa mchezaji ataepangwa katika kikosi kitachoanza kucheza na akaonekana kama moja ya wafungaji bora akifanana na Kylian Mbappé kwa idadi ya magoli mpaka mwezi December 2018.Tarehe 19 January 2019, Emiliano alijiunga Cardiff city ya ligi kuu nchini uingereza kwa kiasi cha euro 15£ milioni. Na kuvunja rekodi za usajiri za klabuni hapo. Ambapo gharama kubwa ilikua ni euro 11£ milioni kwa Gary Medel mnamo 2013.Sala alipewa ofa ya kujiunga na ligi ya nchini china ambayo ingemlipa mshahara mnono lakini kwa kuwa alikua na matamanio ya kucheza soka nchini uingereza yenye ushindani zaidi akakata kwenda china, na kujiunga na Cardiff city Mauti yalipo mkuta.Uchezaji wake ulifananishwa na mshambuliaji mahiri ya klabu ya leicister city, lakini yeye binafsi aliamini kuwa anafuata nyayo za nguli wake aliemkubali Gabrieli Batistuta.Je?, wachezaji wakitanzania na uchezaji wetu tunafuata nyayo za wakongwe gani wakitanzania halisi?, kuna jambo la kujifunza kwa Marehemu Emiliano, moja ni kusimamia misingi ya kile unachikihitaji ili kufanikisha malengo yako, mbili ni kwamba katika soka maslahi sio jambo la msingi, mtu mwenye uwezo mkubwa maslahi humfuata na sio mchezaji kufuata maslahi yake katika klabu flani.Kuweka juhudi katika katika uchezaji ndio mafanikio huanzia hapo. Juhudi haiendi bure, tusikubari kushindwa!.Mwandishi : ISACK MSINJILI

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here