Home Kimataifa Warriors Vs Cavaliers Ni Vita. Lebron na Irving Wafanya Kweli.

Warriors Vs Cavaliers Ni Vita. Lebron na Irving Wafanya Kweli.

3484
0

Inawezekana wengi walishachora mstri mwekundu akiwemo moja ya wanahabari maarufu Stephen A Smith kuwa Golden State Warriors wangetwaa ubingwa katika uwanja wa Cleveland Cavaliers, na kumaliza fainali hizi kwa ushindi wa 4-0 huku wakiwa wamemaliza hatua ya mtoano kwa 16-0. Hata hivyo ushindi wa alama 137-116 wa Cleveland umefuta vyote hivi.

Lakini  hii ni timu yenye Lebron James, ambayo ilikuwa inazungumziwa hapa baada ya kuwa nyuma kwa michezo 3-0. Lebron James alihitaji mchezo huu kuliko mchezo mwingine wowote ili kuokoa wasifu wake wa kuondolewa mara mbili kwenye fainali kw kupoteza michezo 4 yaani SWEEP.

Golden State Warriors yenye Kevin Durant siku zote unategemea itafanya vyema, na ili kuizima unahitaji kuwa bora maradufu dhidi yao. Na hii ni moja ya siku ambazo Cleveland walicheza hivyo na wameturejesha kwenye kumbukumbu za msimu uliopita ambapo walitoka nyuma kwa michezo 3-1 na kuchukua ubingwa.

Lebron akiendelea kufanya vyema akiwa na wastani wa Triple Double, alimaliza mchezo huu akiwa na alama 31, rebound 10 na Assist 11 hku Kyrie Irving akimaliza mchezo na alama 40. Kevin Love aliongeza alama 23 katika mchezo uliokuwa mithili ya vita.

Tofauti na ilivyozoelekea Golden State Warriors walikuwa na Kevin Durant peke yake aliyecheza kama ilivyozoeleka huku Stephen Curry na Kylie Thompson wakipotea kusikojulikana. Curry alimaliza mchezo na pointi 14 huku Klay akimaliza mchezo na pointi 13 pekee. Curry aliingia kwenye mchezo huu akiwa na wastani wa pointi 29 kwa mchezo.

Cleveland walikuwa na mchezo bora baada ya kuongoza mpaka robo ya kwanza kwa tofauti ya pointi 16, 33-49 na ilionekana wazi kuwa leo walijipanga kufanya vyema. Cavaliers walipata asilimia 54 ya mitupo yao ya pointi tatu ikiwa ni mitupo 24 kati ya 45 waliyojaribu huku Warriors wakiwa ovyo kwa kupata asilimia 28 tu ya mitupo ya pointi 3 kwa maana ya mitupo 11 kati ya 39.

Mchezo wa 5 utakuwa  alfajiri ya Jumanne San Fransisco katika uwanja wa Oracle Arena wa Golden State Warriors.

HIGHLIGHTS

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here