Home Kimataifa Warriors Mabingwa, Durant MVP, Mama Afurahia, Lebron Na Rekodi Mbovu.

Warriors Mabingwa, Durant MVP, Mama Afurahia, Lebron Na Rekodi Mbovu.

4217
0

Ilikuwa kama ndoto naam ndoto kubwa ya familia ya Durant. Kevin Durant hakuondoka Oklahoma City Thunder kwa sababu alipenda kuondoka na kwenda kwa Warriors waliowafunga msimu uliopita bali aliondoka kwa sababu aliamini kuwa asingeweza kushinda ubingwa wa NBA akiwa na Russell Westbrook ambaye alipenda kuongoza yeye timu.

Huku kwa Warriors angekutana na Stephen Curry ambaye hakuwa na shida kugawana ustaa na ndio maana kila mchezaji wa Warriors hujihisi ni mwenye umuhimu kikosini.

Machozi ya mama Durant, Wanda Durant yalidhihirisha kuwa waliishinda presha na walikuwa sasa huru kwani hatimaye mwanae ameitwa bingwa. Ndoto imetimia na maandiko yametimia pia, kutoka OKC mpaka Bay Arena kumekuwa na faida kubwa.Naam na mwanae amekuwa MVP wa fainali hizi.

Haya yote ni maelezo unayoweza kuyaweka kwa ufupi ukiwa unazungumzia ubingwa wa Golden State Warriors walioutwaa baada ya kuifunga Cleveland Cavaliers kwa pointi 129-120 na kuweza kushinda katika mchezo wa tano na matokeo kuwa 5-1. Hii inaendeleza rekodi ya Warriors ambayo imeshinda jumla ya michezo 16 na kupoteza mmoja pekee kwenye hatua hii ya mtoano.

Durant ameendelea kuwa na kiwnago bora baada ya kufunga pointi 39 kwenye mchezo huu huku akiweza  kufunga pointi 30+ kwenye michezo yote ya fainali.

Stephen Curry aliongeza pointi 34, na assist 10 pamoja na rebound 6 akimaliza mfululizo wa michezo akiwa na wastani wa pointi 28, assist 9 na rebound 9, kiwango ambacho kinamfanya awe amepanda kiwango kikubwa tofauti na kwenye fainali zilizopita ambapo Cavaliers walishinda katika mchezo wa 7 na kutwaa ubingwa huo.

James, ambaye mwaka 2012 akiwa na Miami waliifunga Oklahoma City Thunder ya Durant kwenye fainali na kutwaa ubingwa alimaliza mchezo akiwa na pointi 41, rebound 13 na assist 8. Hii ni fainali ya 8 kwa Lebron huku akiwa ameshinda 3 na kupoteza 5, na amemaliza fainali hizi akiwa na wastani wa Triple Double.

Kyrie Irving alimaliza mchezo huu akiwa na pointi 26 ikiwa ni baada ya kuiongoza Cavaliers kushinda mchezo wa 4 akifunga pointi 40 lakini alipata mitupo 9 tu kati ya 22 aliyojaribu.

Andre Iguodala, ambaye alitwaa tuzo ya mchezaji bora mwenye thamani kwenye fainali za mwaka 2015 aliibuka tena kwenye mchezo huu wa fainali mwaka huu na kufunga pointi 20 akitokea katia benchi.

HIGHLIGHTS

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here