Home Kitaifa Wambura ashikiliwa TAKUKURU

Wambura ashikiliwa TAKUKURU

2934
0

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura anashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

“Ni kweli yupo tumemshikilia hapa TAKUKURU Dar es Salaam, anatarajia kufikishwa mahakamani leo. Tutamfikisha mahakama ya Kisutu leo, hatujui taratibu zitakuwaje pale mahakamani lakini atafikishwa kuanzia saa 3 asubuhi”-Doreen Kapwani, afisa uhusiano TAKUKURU.

Doreen amesema mambo mengine kuhusu kwa nini wanamshikilia Wambura yatajulikana mahakamani.

Wakati huohuo pia Wambura kupitia wakili wake Emmanuel Muga, ametangaza kuachana na masuala ya uongozi wa mpira wa miguu na kuamua kubaki shabiki na mpenzi kama ilivyo kwa wengine.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here