Home Kitaifa Wakongwe waibeba African Lyon

Wakongwe waibeba African Lyon

2850
0

African Lyon imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliohezwa uwanja wa Uhuru.

Kocha msaidizi wa Lyon Adam Kipatacho amesema ushindi huo unatokana na muunganiko mzuri wa wachezaji wao wazoefu Abdi Kassim, Redondo na Jabir Aziz.

“Tumemuongeza mtu mzima Abdi Kassim ‘Babi’ na ametengeneza muunganiko mzuri na Ramadhani Chombo ‘Redondo’ na Jabir Aziz tunaimani kubwa hata michezo ijayo tutafanya vizuri”- Adam Kipatacho, kocha msaidizi African Lyon.

“Kilichokuwa kinaisumbua African Lyon ni combination na hiyo ilikuwa inatokana na ‘ingia toka’ ya wachezaji.”

Lyon sasa imefikisha pointi 19 baada ya kucheza mechi 22 ikiwa katika nafasi ya 18 katika msimamo wa ligi kutoka nafasi ya 20 kabla ya mchezo wa leo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here