Home Ligi EPL WAKOMBOZI WA UINGEREZA BAADA YA UTUMWA WA MIAKA 15

WAKOMBOZI WA UINGEREZA BAADA YA UTUMWA WA MIAKA 15

788
0

kane-vardy-e1448380217378

Na Athumani Adam

Kwenye msimu wa kwanza ligi kuu England yaani Epl 1992/1993 tano bora ya orodha ya wafungaji ilibeba waingereza. Wakati huo Harry Kane alikuwa kado kuzaliwa, Jamie Vardy alikuwa na takribani miaka mitano.

Hapo alikuwepo Teddy Sheringham aliyekuwa na goli 22, kutoka Nottingham Forest kisha akaenda zake Tottenham Hotspurs. Wengine ni Les Ferdinand wa QPR goli 20, Dean Holdsworth wa Wimbledon goli 19 na Alan Shearer wa Blackburn Rover goli 16

Wakati huo ilikuwa kawaida kwa waingereza kupishana kwenye orodha ya ufungaji bora. Majina ya Andy Cole wa Newcastle United, Robbie Fowler kutoka Liverpool, Ian Wright wa Arsenal, Les Ferdinand yalichomoza kila mara mwanzoni mwa miaka ya tisini kutokana na sababu kuu mbili.

Kwanza hawa watu walikuwa mafundi sana wa kupasia nyavu, tafuta video zao utaamini nachosema. Pili ligi yao haikuwa na wageni wengi kutoka nje ya Uingereza kama ilivyo sasa. ambapo timu kama Man City inaanza kwenye mechi ikiwa na mwingereza mmoja tu, ambaye ni golikipa Joe Hart.

Baada ya waingereza kupotea kwenye safu ya ufungaji bora na kuchukuliwa na wageni kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 2000, msimu huu kama wamefufuka tena. Wana Harry Kane na Jamie Vardy ambao  wanafanya vizuri sana, wapo juu ya msimamo wa ufungaji.

Tayari Kane ameingia kwenye rekodi ya wachezaji watano ambao waliwahi kufunga goli 20 ndani ya msimu miwili mfululizo. Harry Kane amerudia tena kile alichofanya msimu uliopita, bila shaka kuna uwezekano mkubwa wa kuwa tena mwingereza mwingine kutwaa kiatu cha ufungaji bora baada ya miaka 16 kupita.

Uwezo wa Harry Kane kufunga utakata kiu ya waingereza kuona mwingereza mwingine akichukua kiatu tena baada ya Kelvin Philiphs kufanya hivyo mara ya mwisho 2000. Ana kila sababu ya kufanya hivyo, hususani kipindi hiki ambacho wageni wenye majina makubwa kama Sergio Aguero kupungua kasi ya kufunga.

Wengi walijaribu kutafuta kiatu cha ufungaji, lakini haikuwa bahati kwao. Mfano Rooney alijaribu akashindwa kwa Didier Drobga msimu wa 2009/10. Drobga alimaliza na goli 29 wakati Rooney akaishia goli 26

Hata pale mkongwe Alan Shearer akiwa Newcastle United alipo jaribu 2003/04, mambo yakawa magumu mbele ya fundi wa kifaransa, “kichogo” Thiery Henry. Henry alimaliza msimu na goli 30 ambapo Shearer akamaliza na goli 22

Daniel Sturridge akapotea mbele ya mchezaji mwenzake kutoka Liverpoool, Luis Suarez msimu wa 2013/14.

Msimu huu Harry kane pamoja na Jamie Vardy wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa kiatu, hiyo kutokana na uwezo mkubwa wa kupachika mabao. Zimebaki mechi ambazo chini ya 8 msimu kuisha, tunasubiri vitu viwili, kwanza kuona Lecister City au Spurs wakitwaa ubingwa wa EPL.

Pili mwingereza akitwaa kiatu cha ufungaji bora kipindi hiki ambacho ligi imekuwa na wageni wengi kutoka nje ya Uingereza baada ya kuteswa sana na utawala wa kina Jimmy Floyd Hasselbank, Thiery Henry, Nikolas Anelka, Robbin Van Persie, Didier Drogba, Luis Suarez, Sergio Aguero kwa miaka 15 iliyopita.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here