Home Kitaifa Wajumbe wapya TFF wala kiapo

Wajumbe wapya TFF wala kiapo

2883
0

Mkutano mkuu wa mwaka wa TFF ambao umefanyika February 2, 2019 jijini Arusha ni mkutano wa kwanza wa Karia tangu aingie madarakani.

Mkutano huo ulikuwa na ajenda 14 lakini ajenda ambazo zilikuwa nzito ni pamoja na kupitia mapendekezo ya marekebisho katiba ya TFF ili shirikisho kufanya kazi kuendana na mahitaji ya kisasa.

Mkutano huo umefanya uchaguzi wa kuziba nafasi ya Mjumbe wa kamati ya utendaji ya TFF akiwakilisha kanda ya Shinyanga na Simiyu, na Osuri Charles Kosori ameshinda kwa kura 91 akiwapiku Benister Rugora aliyepata kura 20 na Kanjanja Magesa aliyepata kura 17.

Pia Mkutano huo umewaapisha wajumbe wapya wa kamati ya utendaji ambao ni Ahmed Msafir Mgoyi na Athuman Nyamlan ambao wametueliwa na Rais wa TFF, wengine walioapishwa ni Stephen Mguto Mwenyekiti mpya wa bodi ya ligi na Amina Karuma ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha soka cha wanawake Tanzania.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here