Home Kimataifa Waingereza wanasema soka linarudi nyumbani – watauvuka mtihani wa Colombia ๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ด?

Waingereza wanasema soka linarudi nyumbani – watauvuka mtihani wa Colombia ๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ด?

11455
0

Mchezo wa Colombia vs England katika dimba la Spartak Stadium jijini Moscow ndio utakuwa mchezo wa kufunga pazia la 16 bora bora katika 2018 FIFA World Cup Russia.

Colombia hawajawahi kuifunga Three Lions, mchezo wao wa mwisho kabisa kukutana ulikuwa miaka 20 iliyopita katika World Cup 1998 wakati England waliposhinda 2-0.

Vijana wa Jose Pekerman walifuzu hatua ya mtoano kwa kuifunga Senegal katika mchezo wa mwisho wa kundi lao na kumaliza wakiwa nafasi ya kwanza lakini mpaka sasa hawajaonyesha kiwango cha kuridhisha sana.

England ๐Ÿด๓ ง๓ ข๓ ฅ๓ ฎ๓ ง๓ ฟ walishinda mechi zao mbili za kwanza za makundi na leo watawategemea wachezaji Harry Kane, Lingard, Sterling kuwapeleka robo fainali. Mchezo wa mwisho wa makundi uliisha kwa kufungwa 1-0 na Belgium huku kocha Gareth Southgate akiwapumzisha wachezaji wake muhimu. Huu ndio utakuwa mtihani mgumu wa kwanza wa Southgate.

Hali ya Vikosi:

Dele Alli yupo fiti kuanza leo baada ya kukosa mechi mbili za mwisho za makundi vs Panama na Belgium. Gareth Southgate anatarajiwa kuwarudisha kikosini wachezaji aliowapumzisha dhidi ya Belgium akiwemo nahodha Kane ambaye mpaka sasa magoli 5.

Colombia bado wana wasiwasi na utimamu wa kiafya wa James Rodriguez, ambaye alipata majeraha katika mchezo dhidi ya Senegal. Anaweza kuanzia benchi.

Kiungo mwenzake Wilmar Barrios anaweza kupewa nafasi ya kuanza badala yake.

Head to Head

โ€ข England hajawahi kupoteza mechi dhidi ua Colombia katika mechi 5 walizowahi kukutana. Michael Owen alifunga hat trick katika mechi yao ya mwisho kirafiki waliyokutana ambayo iliisha kwa 3-2 jijini New Jersey mwaka 2005.

โ€ข Three Lions waliwafunga Colombia 2-0 katika mchezo pekee wa kombe la dunia uliowakutanisha kwenye mashindano haya – magoli ya Darren Anderton na David Beckham katika hatua ya makundi mwaka 1998.

๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ด Colombiaโ€ข Hii ni mara ya 3 kwa Colombia ๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ด kufuzu kucheza hatua ya mtoano. Mara 1 tu wamefanikiwa kuvuka hatua hii – ilikuwa miaka 4 iliyopita nchini Brazil.

โ€ข Hawajafungwa katika mechi 8 dhidi ya timu za ulayabtangu kocha Jose Pekerman alipoanza kuifundisha timu hii mwaka 2012 (Wakishinda 6, Sare 2).

โ€ข Los Cafeteros wamefunga katika kila mechi katika michezo 8 iliyopita ya World Cup – timu ya mwisho kuwazuia kufunga katika michuano ilikuwa England mwaka 1998.

England ๐Ÿด๓ ง๓ ข๓ ฅ๓ ฎ๓ ง๓ ฟโ€ข England wameshinda mechi 2 kati ya 8 zilizopita za hatua ya kutoana kwenye World Cup.

โ€ขUshindi wao wa mwisho katika hatua ya kutoana kwenye World Cup dhidi ya taifa la Amerika ya Kusini ulikuwa dhidi ya Ecuador 1-0 katika raundi ya 16 bora mwaka 2006.

โ€ข England wameshindwa kufunga katika mechi 1 tu kati ya 18 za hatua ya mtoano katika World Cup – mchezo huo ulikuwa wa sare tasa dhidi ya Portugal mwaka 2006 katika robo fainali – Portugal walishinda kwenye penati.

โ€ข Harry Kane amecheza dakika 153 tu za Kombe la dunia lakini tayari amefunga magoli 5, akizidiwa na Gary Lineker pekee mwenye magoli 10.

โ€ข Huu ni mchezo wa 18 wa Uingereza dhidi ya mataifa ya Amerika Kusini katika World Cup – wameshinda 8, sare 3 na wamefungwa 6.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here