Home Kitaifa Wachezaji waachwa kwenye mataa bila nauli

Wachezaji waachwa kwenye mataa bila nauli

4302
0

Wachezaji wa Nyundo FC inayoshiriki kombe la TFF wamejikuta wakitelekezwa na mwenyekiti wa timu Shabani Rashid wakiwa Sumbawanga mkoani Rukwa baada ya kutoka kwenye mchezo wao dhidi ya Living Stone ya Njombe kwa madai kuwa ameishiwa pesa aliyopewa kutoka kwa mdhamini wa mashindano.

NAHODHA WA TIMU: “Viongozi hawakuwa pamoja na sisi, hadi tunafika nyumbani hatuna simu mifukoni hatuelewi tunafanyaje watu wametutelekeza”-Joseph Stephano.

KOCHA: Tumetoka Sumbawanga hatuna nauli wala chochote, kiongozi tuliyekuwa nae tulitarajia atulipie nauli katukimbia na chama cha mpira Katavi wanadai walimtumia lakini yeye hatujamuona tumefika hapa kwa tabu simu zetu zimezuiliwa kwenye basi”-Geoffrey Bernard.

MWENYEKITI CHAMA CHA SOKA KATAVI: “Sisi kama viongozi wa chama cha mpira cha mkoa tulishirikiana na chama cha mpira manispaa na tulimtumia pesa mwenyekiti wa timu ya nyundo Bw. Rashid na alizipata na aliongozana na timu”-Emanuel Chaula.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here