Home Kitaifa Wachezaji wa Mtibwa Sugar majaribioni nje ya nchi

Wachezaji wa Mtibwa Sugar majaribioni nje ya nchi

3837
0

Kocha wa Mtibwa Sugar amethibitisha baadhi ya wachezaji wake kupata fursa ya kwenda kufanya majaribio nje ya nchi.

“Baadhi ya wachezaji wameenda kufanya majaribio kipindi cha mechi zetu mbili zilizopita, waliofanikiwa bado taarifa rasmi hazijaja.”

“Kelvin Sabato bado yupo South Africa, Jafar Kibaya na Juma Liuzio bado walikuwa Dar wanatafuta Visa za kwenda Misri, Dickson Job ameenda Nairobi kutafuta Visa ya Ukraine.”

“Kuna baadhi wamekosa Visa (Jafar na Juma) wanaweza wakarudi lakini Job na Kelvin mambo yao yanaendelea vizuri.”

“Mimi nafurahi kuona wanapata fursa za kwenda nje, endapo wataondoka ndio fursa inafunguka kwa wachezaji wengine kupata nafasi Mtibwa.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here