Home Kitaifa Wachezaji 10 wakigeni VPL sio ishu, ishu inaanzia hapa…!

Wachezaji 10 wakigeni VPL sio ishu, ishu inaanzia hapa…!

9744
0

Rais wa TFF Wallace Karia ametoa ufafanuzi juu ya kilichopelekea TFF kufanya marekebisho ya kanuni za ligi kuu ikiwa ni pamoja na kjongeza kioengele cha wachezaji 10 wa kigeni jambo ambalo linaonekana kupokelewa tofauti na wadau wa soka nchini.

Karia amefafanua jambo ambalo limekuwa na mjadala mpana sana kuhusiana na idadi ya wachezaji 10 wa kigeni kusajiliwa na timu kwa msimu mmoja.

Watu wengi wamekuwa wakilalamika kwamba athari kubwa ya kuongeza idadi ya wachezaji wa kigeni itaathiri ubora wa timu yabtaifa kwa sababu timu zenye uwezo wa kupata michezo ya kutosha na kuwaandaa wachezaji vizuri ndio zenye uwezo wa kusajili wachezaji 10 wa kigani.

Wadau wanahoji endapo wachezaji 10 wa kigeni wakitumika kila mechi, je wachezaji wetu wa timu ya taifa wwanaocheza ligi ya ndani wataweza kukidhi mahitaji ya kuifanya timu ya taifa iwe bora?

Sisi sote ni mashahidi hivi hata tukiondoa wachezaji wote wa kigeni, ligi yetu ikawa na wachezaji wa nyumbani tu, je tutaweza kuwa na timu ya kushindana na kufuzu AFCON au kombe la dunia?

Kwa hiyo lazima twende na namna ambavyo dunia inakwenda, kama sisi tunachelewa katika baadhi ya maeneo tuchue kama changamoto. Kwenye dunia tuliyopo kila kitu kimekuwa biashara, soka imekuwa biashara kwa 100% mwenye uwezo acheze iwe changamoto kwa wachezaji wetu.

Wachezaji wetu wengi hawajui kwa nini wanacheza mpira, walio wengi wanafikiri kucheza ni sehemu ya kupoteza muda. Kwa hiyo iwe changamoto kwao kujituma na kucheza kwa malengo.

Wageni wanaokuja kucheza kwetu ukifatilia malengo yao utagundua wanakuja kucheza Tanzania kama sehemu ya kupata nafasi ya kutengeneza CV ili watoke kwenda sehemu nyingine.

Soko la Ulayanna Asia nafasi zinazidi kuwa finyu kwa sababu tunaona wachezaji wengi kutoka mataifa ya Ulaya wanavyokwenda Asia ambako wanazidi kuipandisha thamani ya soko.

Wachezaji wetu tunajua wengi wao ni wavivu hawajitumi! Tunawafahamu hakuna haja ya kuanza kutaja mmoja baada ya mwingine.

Kwangu mimi timu moja ya VPL kuwa na wachezaji 10 sio ishu, ishu ni hao wachezaji 10 ni wa viwango gani? Tunategemea wachezaji wanaokuja wawe na uwezo kuliko wachezaji wazawa.

Unaposajili mchezaji wa kigeni maana yake hakuna mchezaji wa kiwango hicho kwa hapa nyumbani.

Vilabu ambavyo vina uwezo wa kusajili wachezaji 10 kikichukua ubingwa wa VPL na kupata nafasi ya kwenda kushindana na vilabu vingine na kupata mafanikio mwisho wa siku vilabu vya Tanzania ndio vinakuwa vimefanikiwa.

Jambo muhimu la kufanyia kazi ni aina ya wachezaji wanaokuja, wawe wachezaji haswa. Endapo vigezo vitazingatiwa, italeta mantiki ya kuruhusu wachezaji 10 lakini tusifungue tu milango wakajazana wachezaji ambao wakawaida au wazee wanaokuja kumalizia mpira jambo ambalo halitakuwa na maana.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here