Home Ligi BUNDESLIGA Vilabu Vya La Liga Vyakosekana Kwenye Orodha Ya Wingi Wa Mashabiki Viwanjani.

Vilabu Vya La Liga Vyakosekana Kwenye Orodha Ya Wingi Wa Mashabiki Viwanjani.

8900
0

Inawezekana kabisa vilabu vya Hispania vikawa katika kiwango bora hasa wanaposhiriki michuano ya Ulaya Ubora huu hutakiwa kuchochea kuwepo kwa mashabiki wengi wanaoudhuria michezo inayohusisha vilabu vyao pia.

Lakini isivyotarajiwa washabiki wa La Liga wameendelea kuonekana wenye mahudhurio machache zaidi hata kwa vilabu kama Real Madrid na Barcelona na hata Atletico Madrid kwa kulinganisha wastani wa uwezo wa uwanja na washabiki wanaoingia.

Ifuatayo ni orodha ya Viwanja vilivyokuwa na wastani mkubwa wa watazamaji kwa vilabu vya Ulaya.

1. Allianz Arena

Uwanja huu umeingiza asilimia 100 ya mauzo ya tiketi za kila mchezo, hivyo Bayern wameuza tiketi zote 75000 za kila mchezo msimu huu.

2. Schwarzwald-Stadion

Huu ni uwanja wa nyumbani wa klabu ya SC Freiburg na una wastani wa watu 23,942 kwa mchezo, ikimaanisha ni siti 58 pekee zinazobaki wazi kwa kila mchezo.

3. Stamford Bridge

Uwanja unaoingiza wastani mkubwa zaidi wa mashabiki kwa England, ikiwa ni mashabiki 41,528 kati siti 41,631 zilizopo. Ikiwa ni siti 103 pekee zinazobaki wazi kwa kila mchezo.

4. Emirates Stadium

Asilimia 99.55 ya uwanja huu inajaa mashabiki. Yaani mashabiki 59,998 wanaingia uwanjani kwa kila mchezo.

5. Old Trafford

Uwanja wa nyumbani wa klabu ya Manchester United, unaingiza mashabiki 75,288 kwa kila mchezo kwenye uwanja wenye uwezo wa kubeba mashabiki  75,643.

6. King Power Stadium

Kila shabiki wa Leicester alikuwa na hamu kubwa ya kushuhudia klabu hii ikitwaa ubingwa, wanaingiza mashabiki 31,948 kwa kila mchezo.

7. RheinEnergieStadion

Huu ni uwanja wa klabu ya FC Koln, unabeba washabiki 50,000 na umefanikiwa kuingiza washabiki 49,983 kwa wastani.

8. Goodison Park

Mipango yao ya kujenga uwanja mpya wa River Mersey inaeleweka ikizingatia kuwa klabu ya Everton inaingiza mashabiki 39,032 kwenye uwanja wa Goodison.

9. Sherlust Park

Crystal Palace wamefanikiwa kuuza asilimia 98.52 ya tiketi za uwanja wao kwa kila mchezo unaopatikana kusini mwa London kwa kila mchezo.

10. Bet365 Stadium

Timu nyingine kutoka ligi kuu ya Uingereza, Stoke imeuza jumla ya siti 27,400 kati ya siti 27,932 za uwanja wao kwa kila mchezo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here