Home Dauda TV Vilabu vya Bongo vinaacha Mil 70 SportPesa, ligi haina mdhamini!!

Vilabu vya Bongo vinaacha Mil 70 SportPesa, ligi haina mdhamini!!

2944
0

Mwandishi na mchambuzi wa michezo Tanzania Charles Abel amesema vilabu vya Bongo vilizidiwa uwezo na timu za Kenya kwenye mashindano ya SportPesa yaliyomalizika mwaka huu 2019.

Charles anasema haamini kama vilabu vya Tanzania vinaweza kuacha mzigo wa zaidi ya shilingi milioni 70 za kibongo ndani ya siku 6 huku vikicheza ligi ambayo haina mdhamini na bingwa hajulikani atapata nini.

Kwa hiyo Charles anaamini vilabu vya Tanzania vilitaka kushinda ubingwa wa SportPesa 2019 na kuvuna mzigo huo lakini vilizidiwa uwezo na vilabu vya Kenya ambapo timu zote za Tanzania zilitolewa na vilabu vya Kenya ambavyo vilifanikiwa kucheza fainali.

“LigiKuu Tanzania bara hadi sasa hivi mdhamini hajulikani na bado zawadi kwa bingwa haijulikani lakini mashindano ya SportPesa yanachezwa ndani ya siku 6 bingwa anapata zaidi ya Tsh.70m, sitaki kuamini kama timu itaacha kutolea macho kiasi kikubwa cha pesa kwa siku chache. Timu zetu zilizidiwa”-Charles Abel, mwandishi wa michezo Tanzania.

Full interview tayari ipo #YouTube
kwenye account yangu ya #DAUDATV
pita hapo ukutane na maoni ya #Mwandamizi Charles Abel

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here