Home Dauda TV Video: Manula kumfuata Bocco Simba?

Video: Manula kumfuata Bocco Simba?

31435
0
Golikipa wa Azam FC na timu ya Kilimajnaro Stars Aishi Manula

Wakati John Bocco akihusishwa kujiunga na klabu ya Simba baada ya kumaliza mkataba wake Azam kumekuwa na story nyingi zikiwahusu wachezaji wengine wa Azam (Aishi Manula na Shomari Kapombe) wakitajwa kutakiwa na wekundu wa Msimbazi.

Dauda TV ilimnasa Manula kwenye hafla ya utoaji wa tuzo za VPL 2016/17 na kupiga nae story kuhusu kuhusishwa kujiunga na Simba lakini akasema hizo ni tetesi, yeye bado ana mkataba na Azam na yupo kwenye mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo ili kuongeza mkataba mpya kuendelea kuhudumu Azam FC.

“Hizo ni tetesi zinavuma lakini mimi bado nipo Azam japo mkataba wangu unaelekea ukingoni lakini naamini bado nitaendelea na Azam na tumeshaanza mazungumzo kwa ajili ya mkataba mpya,” alisema Manula.

Wakati huohuo, afisa habari wa Azam FC Jafari Idd amethibitisha kwamba, klabu ya Azam imeachana na Bocco baada ya mkataba wa mkongwe huyo kumalizika.

“John Bocco mkataba wake umekwisha kwa mujibu wa bodi ya Azam na uongozi hautaendelea na Bocco kwa hiyo anakuwa ni mchezaji huru, hivyo anauhuru wa kuamua aende wapi ndani au nje ya nchi.”

“Sisi kama Azam klabu tunamtakia kila la heri anapokwenda, ameitumikia timu kwa muda mrefu na kuwa seheu ya mafanikio ya timu tangu wakati timu ikiwa inapambana kupanda daraja mpaka tunakwenda kucheza michuano ya kimataifa kwa hiyo hatutamsahau  kwa mchango wake.”

“Lolote linalomhusu Bocco kwa sasa ni vizuri akatafutwa mwenyewe anaweza kueleza yuko wapi au anakwenda wapi kwa sababu ni maamuzi yake mwenyewe.”

Idd pia akazungumzia hali ilivyo kuhusu Manula na Kapombe kama wataendelea kuwepo Azam au wataondoka kama ambavyo taarifa zinazidi kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

“Manula na Kapombe haijamalizika kama ilivyo kwa Bocco , wao bado wana muda wa kubakia Azam kwa mujibu wa mikataba yao. Hadi sasa uongozi bado haujaniambia kuhusu hilokwa hiyo siwezi kutangaza mkataba wamtu umebaki muda gani kwa sababu ni siri kati ya mchezaji na waajiri wake.”

“Hadi sasa ni Bocco hakuna mtu mwingine ambaye tumempa barua ya mkono wa kwaheri.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here