Home Kimataifa Victor Moses apigwa mkwara Nigeria

Victor Moses apigwa mkwara Nigeria

4189
0

Kocha mkuu wa Nigeria Gernot Rohr amesema milango ipo wazi kwa nyota wao wa zamani Viktor Moses kurudi timu ya taifa.

“Viktor ni mchezaji mkubwa sana ndani ya taifa. Alistaafu soka la taifa baada ya kombe la dunia. Tunaheshimu sana maamuzi yake. Lakini kama ataona umuhimu wa kurudi hapa sina tatizo na hilo” Rohr

“Lakini Moses kama anataka kurudi anapaswa kupambana kwa hali na mali. Nigeria ya sasa sio lelemama.”

“Tumekamilika kila idara. Tupo fiti na kikosi chetu kimejitosheleza vilivyo licha ya kwamba hatuwezi kudharau uwezo wa Moses lakini pia hatuwezi kumlazimisha arudi”

“Tuna wachezaji wengi wenye uwezo wa kariba sawa na yake tu, akina Ahmed Mussa, Alex Iwobi, Samuel Chukwueze, na Samwel Kalu”


Victor Moses amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga klabu ya Fernabache kwa mkopo akitokea darajani


KWINGINEKO

Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Ghana Maxwell Konadu amesema haoni wa kumzuia Asante Kotoko kufuzu katika hatua ya makundi.

Asante wapo kundi moja na Al Hila kutoka Sudan, Zesco ya Zambia, na Nkana FC.

“Nawapongeza sana Asante kwa kuwa wamedhihirisha kuwa wao ni klabu bora Ghana na hapa barani Afrika”

“Katika hatua hii kila klabu ni bora lakini nina imani kubwa sana na Kotoko” Konadu

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here