Home Ligi BUNDESLIGA Utakatifu wa namba 7 unavyomuingiza Mbappe katika kundi la Cr7, Beckham na...

Utakatifu wa namba 7 unavyomuingiza Mbappe katika kundi la Cr7, Beckham na Frank Ribery

14164
0

Namba saba katika ukristo, Saba katika dini ya wenzetu wakristo ni namba takatifu na ndio sababu mungu aliwaambia wafanye siku zote kazi ikifika ya 7 wapumzike kwa sababu hiyo ni siku ya mungu.

Na kama hufahamu tu ni kwamba mtawala wa soka duniani kwa sasa anavaa namba 7 na amelitawala soka kwa takribani miaka zaidi ya mitatu na kama mambo yakimuendea poa bado ana muda wa kuendelea kutawala tena ni Cristiano Ronaldo.


Mchezaji bora chipukizi wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 Kylian Mbappe ambaye baada ya kung’ara kombe la dunia amepewa jezi yenye namba takatifu jezi namba 7, jezi ambayo pia ndio inavaliwa na Role Model wake(Cristiano Ronaldo).

Mbappe aliyekuwa anavaa namba 29 sasa atakuwa akivaa namba 7 ambayo hapo kabla ilikuwa ikivaliwa na winga wa Kibrazil Lucas Moura aliyetimkia Tottenham Hotspur.

Katika historia ya soka namba 7 inaonekana ni namba ambayo imebarikiwa kuvaliwa na nyota wengi wenye vipaji vikubwa ulimwenguni na kwa uchache tuwaone hawa 10 ambao nao wamepitia katika namba hii.

1. George Best. Hapa wengi hatukuwa tumezaliwa, lakini unaambiwa Best alikuwa Best haswa kwani alikuwa akipiga na miguu yote na mabeki walikuwa wanamkimbia, katika michezo yake 470 alifanikiwa kuweka kambani mabao 179 na hadi sasa ni kati ya nyota wanaoheshimiwa Unuted na gwiji wa Brazil Pele amekiri kwamba Best ndio mchezaji bora amewahi kumuona.


2.Luis Figo. Kati ya viungo bora kabisa kuwahi kutokea duniani, Figo alikuwa mzuri kukaa na mpira na kuamua uende wapi ni kati ya nyota wakubwa sana kuwahi kutokea Ureno na katika wakati wake timu ya taifa alipiga mabao 32 katika michezo 127 na akiwa na jumla ya assists 106 katika La Liga.

3.David Beckham. Muingereza mwingine ambaya aliinyanyasa dunia akiwa na jezi namba 7, David yule wa United alikuwa ni moto haswa na alitisha zaidi katika mipira iliyokufa na ndicho wengi tunamkumbuka nacho, katika mechi 265 kwa United alifanikiwa kufunga mara 62.


4.Frank Ribery. Kama ilivyo kwa Mbappe ambaye ni hatari akicheza kutoka pembeni, baasi kuna huyu Frank Ribery ambaye majeruhi yanamsumbua sumbua Bayern lakini ni nyota mkali mwingine mwenye 7 mgongoni, michezo 248 Bayern ameshawafungia mabao 80.


5. Eric Cantona. Mfaransa mwingine ambaye amewahi kuisumbua dunia na jezi namba 7, sahau kuhusu “kung fu kick” aliyompiga shabiki lakini Cantona alifanikiwa kufunga mabao 64 katika mechi 143 United lakini pia amefunga mabao 131 wakati akikipiga katika ngazi ya vilabu.


6. Andriy Shevchenko. Huyu ndio mcheka na nyavu wa muda wote katika timu ya taifa ya Ukraine akiwa ba mabao 48 lakini vile vile Shevchenko amefunga mabao 68 katika Champions League yanayomfanya kuwa namba 5 katika orodha ya wafungaji bora wa mda wote wa michuano hiyo.


7.Raul Gonzalez. Ndio anashika nafasi ya pili katika ufungaji kwenye La Liga akiwa na mabao 323 na pia ndio mfungaji namba 3 kwa ufungaji katika Champions League akiwa na mabao 71 Raul ameshashinda La Liga pia ameshinda Champions League na namba 7 mgongoni.


8.Roberto Pires. Gwiji wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa, kama ilivyo kwa Mbappe huyu naye alishinda kombe la dunia 1998 na mwaka 2001 alikuwa mchezaji bora wa michuano ya Fifa Confedaration.

9.David Villa. Msimu wa 2005/2010 akiwa na Valencia alifunga mabao 108 akiwa na namba 7, akaenda Barca akapewa namba 7 akafunga mabao 33 kwa misimu miwili kisha Atletico Madrid alikofunga mabao 13 kwa msimu mmoja kabla ya kwenda Marekani lakini pia alivaa namba 7 wakati Hispania wakibeba kombe la dunia pale South 2010.


10.Kenny Danglish. Kocha na mchezaji wa zamani wa Liverpool, huyu alikuwa mnyama haswa uwanjani. Katika mechi 559 katika ngazi ya vilabu Danglish alifunga jumla ya mabao 230 na ameshashinda makombe karibia yote katika ngazi ya vilabu akiwa na Liverpool na jezi namba 7.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here