Home Ligi BUNDESLIGA USITHUBUTU KUPITWA NA VITA YA TOP 4 BUNDESLIGA WEEKEND HII

USITHUBUTU KUPITWA NA VITA YA TOP 4 BUNDESLIGA WEEKEND HII

664
0

Bundesliga-logoNa Simon Chimbo

Haihitaji ufundi kwa mtu wa soka kujua kuwa itakua ni ‘Super Weekend’ katika ligi kuu soka nchini Ujerumani, Bundesliga Jumamosi hii na kuwa ni mchana wa kutokukosa, ni mechi zinazowakutanisha wababe wa juu kabisa katika msimamo wa ligi hii inayopanda kwa kasi hivi sasa.

Borrusia Monchengladbach iliyozaliwa upya hivi sasa watakuwa wakiwakaribisha mabingwa watetezi na vinara wa ligi hiyo hivi sasa Bayern Munich, huku washindi wa pili katika msimu uliopita Vfl Wolfsburg wakikabiliana na timu inayoshika nafasi ya pili hivi sasa timu ya Borrusia Dortmund, ni mchana adimu sana.

GLADBACH KATIKA ‘CHORUS’ 

Ni miongoni mwa timu zilizokua mkiani mwanzoni mwa msimu, Gladbach chini ya Andre Shubbert wana kila sababu ya kuamini wanaweza fanya kitu tofauti dhidi Bayern Munich Jumamosi hii kutokana na kutopoteza michezo 9 mfululizo hadi sasa huku, wakishinda 7 na kutoka sare michezo 2, hawajafungwa.

Monchengladbach ni timu ya pili kwa ubora hivi sasa katika ligi kuu Bundesliga nyuma ya Bayern Munich na kuifanya mechi kati ya timu hizi kuwa si ya kukosa hata kidogo.

Gladbach ndio iliyokua timu pekee msimu uliopita kuizuia Bayern ya Pep Guadiola, baada ya kupata sare tasa katika uwanja wao wa nyumbani, kabla ya kuwafunga Bayern 2-0 mjini Munich.

DORTMUND NA VITA YA UBINGWA

Bayern Munich isingekua hapo ilipo kama kusingekua na ushindani. Pamoja na ukweli kuwa wamepoteza points katika mchezo mmoja tu msimu huu dhidi ya Entranct Frankfurt lakini magoli 5 ya kipindi cha pili yaliyofungwa na mshambuliaji Robert Lewandowski dhidi ya Wofsburg katika dakika 9 tu yanaonesha ubora wa kikosi hiki cha Pep Guadiola.

Kwa upande wao Borrusia Dortmund, pamoja na kupoteza mchezo wao dhidi ya Bayern Munich na kupata sare kadhaa, wamerudi katika upepo huku wakishinda michezo 5 na kupata sare moja tu katika michezo sita mfululizo.

Fomu ya mpachika mabao raia wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang aliyefunga magoli 17 katika michezo 14 ni kitu kinachowapa nafasi nzuri Borrusia Dortmund kumfukuzia Bayern Munich, pamoja na gepu la points 8 baina yao.

FORTRESS WOLFSBURG 

Vfl Wolfsburg hawako katika ubora wao waliokua nao msimu uliopita walipomaliza nafasi ya pili msimu ulipita. Lakini timu hiyo haijapoteza katika michezo 29 wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Volkswagen arena, na wanatarajia kuweka rekodi ya kutopoteza katika michezo 30 endapo tu watawazuia Borrusia Dortmund wasipate ushindi Jumamosi hii.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here