Home Uncategorized Unai alimpiga bao Potchettino kwenye hili

Unai alimpiga bao Potchettino kwenye hili

5809
0

Baada ya mechi ya Arsenal na Tottenham, kumalizika jana, nilitaka kusikia nini ambacho kocha wa Tottenham Mauricio Potchettino atasema. Potchettino alisema, ” Kilichochangia timu yake kufungwa, ni kutokana na kuwa na ratiba ngumu ndani ya siku saba. Yani kucheza mechi tatu ngumu ndani ya wiki moja.Akasisitiza kabla ya mechi dhidi ya Arsenal, walicheza na Chelsea kwenye Ligi Kuu wakapata matokeo, halafu katikati ya wiki wakacheza na Inter milan kwenye mechi ya Ligi ya mabingwa Ulaya.Akaendelea kusema kwamba, Arsenal hawakuwa na ratiba ngumu maana walicheza na Bournermouth halafu katikati ya wiki wakacheza na Vorskia Poltava kwenye Uropa ligi. Hivyo wachezaji wake hawakuwa fiti asilimia miamoja kucheza mechi ya Arsenal.Nirudi kwenye mada husika kwamba mpira ni mbinu na kufanya maamuzi kwa wakati sahihi. Kwa namna moja au nyingine unaweza kuamini mtazamo wa Potchetino au usiamini. Baada ya Tottenham kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza 2-1, dhidi ya Arsenal, wachezaji wake walikuwa mchezoni lakini Potchetino hakuweza kureact haraka mara baada ya Arsenal kusawazisha goli na kuwa 2-2Kuna muda inabidi ubadilike wakati mchezo unaendelea.Kocha Unai Emery wa Arsenal alifanya mabadiliko mawili ya haraka kabla hata kipindi cha pili hakijaanza. Mabadiliko yaliyoipa faida Arsenal.Safu ya ulinzi ya Tottenham ilikuwa inaongozwa na Jan Vertonghen. Unajua kwamba Vertonghen alikuwa hajaanza mechi yoyote ya Spurs miezi miwili iliyopita? Inamaana hakuwa fiti, lakin alijitahidi kuficha madhaifu ya kinda Foyth kutokana na uzoefu wake. Mpira mara myingi ni mchezo wa makosa kila mtu anajua. Lakin kwanini baada ya Arsenal kusawazisha goli na kuwa 2-2, Potchetino hakufanya mabadiliko ya haraka kwa kumuingiza Toby Alderweired? Binafsi naamini kama baadhi ya wachezaji wako unaowategemea sio majeruhi kwanini usiwaanzishe kwenye mechi muhimu au wakaingia hata kipindi pili kufanya mabadiliko? Foyth bado ni kijana mdogo sana anahitaji kujifunza. Kama alicheza vizuri dhidi ya Morata au Giroud, usiwe na uhakika kama atacheza vizuri pia dhidi ya Lacazette na Aubermeyang. Kuwakaba Lacazzete na Aubermeyang unahitaji uzoefu wa Toby Alderweired.Namna ambavyo kocha Unai Emery alivyokuwa anafanya mabadiliko ulikuwa unaona kabisa ni mabadiliko na maamuzi ya kimbinu zaidi( tactical decision) kwa wakati sahihi. Ni kweli Tottenham wanahitaji kuongeza wachezaji lakin Unai Emey kwenye kikosi chake cha Arsenal, wachezaji wote walioanza karibu wote aliwakuta kasoro Lucas Torreira tu ambaye amemsajili msimu huu. Potchetino kama anahitaji kupiga hatua, basi inatakiwa abadilike ili kuifikisha Spurs kwenye mafanikio zaidi.By Patrick Admila

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here