Home DOKUMENTARI UKURASA WA 1: Huyu ndiye Nadir Haroub “Canavaro”

UKURASA WA 1: Huyu ndiye Nadir Haroub “Canavaro”

8021
0

“Ilikuwa mechi ya Simba na Yanga. Mchezo ulikuwa mgumu sana. Viatu vilikuwa vinatembea sana uwanjani. Mwamuzi alionekana kuzidiwa kabisa mchezo kutokana na kila mchezaji alikuwa amekwisha kutibuka. Nilimfuata mwamuzi na kumweleza kwamba mchezo utaharibika. Wachezaji wote wa Yanga walikuja kwa shari shari wakati naongea na mwamuzi. Ni mchezaji mmoja tu alikuwa akijaribua kutuliza munkari ya wachezaji wenzake. Wengine wote vichwa vilikuwa Moto”

“Baadae kidogo nikaumizwa nikawa nagaragara chini mpira ulikuwa kwenye eneo la hatari la timu yetu. Mashabiki wakaanza kupiga kelele wakitaka mpira utolewe nje wala hakuna mchezaji wa Yanga aliyekubali kufanya hivyo. Canavaro akatoka nyuma kwa kasi na kuomba pasi akiwa anajua wazi kuwa timu yake inakwenda kushambulia alituliza mpira na kumsihi mwamuzi aje kunijulia hali hali. Yeye akiwa mtu wa kwanza kabisa kunifuata nikiwa chini. Nilishtuka sana. Nilishangaa Canavaro huyu ametoa wapi moyo ule” Ulimboka Mwakingwe.

Hayo yalikuwa maneno ambayo Mwakingwe alijaribu kumuelezea kwa namna Nadir Haroub alikuwa tofauti kabisa na wachezaji wengine.

Mwanamuziki wa mziki wa kizazi kipya Maarufu kama G nako amesema Yanga imepoteza shujaa wa kweli na mchezaji aliyejua nini maana ya kitambaa cha unahodha.

“Nakumbuka aliwahi kutuokoa mara kadhaa, alikuwa mpambanaji ambaye alisimama nyuma ya Yanga katika mazingira yote”

Mwaka 2006 wakati Canavaro anaitwa timu ya taifa ya Tanzania alionekana kutokuaminika kabisa. Wengi walisema anacheza rafu na alikuwa akisababisha madhara sana.

“Watu wamashindwa kutofautisha kati ya mchezaji anayetumia nguvu na mchezaji anayecheza rafu. Huwa najiona mimi kila mara napomuona Canavaro. Amelitendea haki jina la Canavaro. Ni mchezaji ambaye ametembea vyema kwenye nyayo zangu” Alisema Boniface Pawassa

Moja ya jambo la kukumbukwa zaidi kwa Canavaro ni kijituma.

“Wachezaji wengi wa kizazi hiki hawana uwezo wa kucheza kwa miaka 4 au mitatu mfulilizo hasa katika ubora wao ule ule. Ni wachezaji wachache sana nimeoma wana kariba hiyo labda Kelvin Yondani. Canavaro amedumu kwenye ubora wake kwa zaidi ya miaka 10” Alisema Ally Mayay Tembele.

Pamoja na kwamba kwenye timu ya taifa palikuwepo na ufinyu mkubwa wa nafas, jambo ambalo Canavaro hakulipenda ni kuwadharau wachezaji ambao walikuwa wanaachwa benchi. Hapendi kabisa kuona mchezaji mwingine akionekana hawezi hata kama ni kwa utani.

“Tulikuwa kambini timu ya taifa, pakatokea sintofahamu kambini ingawa sikumbuki vyema shida ilianzia wapi lakini ugomvi ulimhusisha Yondani.

Yondani alishikwa na hasira sana, mimi binafsi nilikerwa sana na kitendo kile. Wakati ule kocha alikuwa Marcio Maximmo. Canavaro ndiye mtu pekee ambaye alichukulia suala lile kimasikhara na akalifanya kama utani. Aliishia kututania sisi wengine mwisho wa siku wote tukajikuta tunacheka na shida kuisha”

“Canavaro alikuwa hapendi dharau hata kidogo. Mtu akiwa benchi anapenda aheshimiwe sawa tu na yule aliyepo uwanjani. Hapendi tabia ya wachezaji wanaopata nafasi kukataa kutolewa au wao kujiona bora kuzidi wale waliopo benchi” Ulimboka

Canavaro aliteka hisia za mashabiki wa Pande zote hata wale wa msimbazi.

“Mimi ni shabiki haswa wa Simba lakini Canavaro ameitendea haki Yanga na Taifa Stars. Huyu ndiye mchezaji aliyetusumbua zaidi kwenye mechi za watani wa jadi” Mwanamuziki Joh Makin

“Mimi binafsi sio mfuatiliaji sana wa mpira, lakini nimekuwa nikisikiliza mpira redioni. Kila mara jina lake linapotajwa hata kama wewe sio mfuatiliaji wa mpira utagundua ni kijana machachari sana. Sijawahi kumuona sana lakini jina lake libeba heshima fulani ya kishujaa” Mwanamuziki Ben Pol.

Kuna wachezaji wamekuwa na tabia ya kubweteka kwa kuwa wana vipaji. Aidha kwa kupumbazwa na maneno ya mashabiki au sifa wanazomwagiwa na wadau wa soka au watangazaji wa mpira. Wanajisahau na mwisho wa siku vipaji vyao vinakufa.

“Shida sio kipaji. Kipaji pekee sio kitu kama mtu asipojituma. Hiki ni kitu kinachowashinda wachezaji wengi. Sasa kwa mantiki hiyo Canavaro ni mtu wa kuigwa. Amedumu na uwezo wake kwa miaka zaidi ya 10” Ally Mayayi

Wachezaji wanapaswa kuchagua maisha ya kuishi. Wapo wachezaji wanajisahau wanakuwa hawana tofauti na wahuni ni kana kwamba kipaji chao ni sawa na pete ya dhahabu kwenye pua ya Nguruwe.

Nidhamu pia imekuwa tatizo kubwa kwa wachezaji wetu. Canavaro alichagua maisha ya tofauti. Ana haki ya kupewa heshima kubwa sana ndani ya Yanga kwa namna alivyoitumia klabu yake. Kuna uwezekano mkubwa kwamba mara kadhaa alikosea lakini hatuwezi kumweka kundi la wachezaji wenye nidhamu mbovu.

Mayayi anamweka Canavaro kwenye kundi la wachezaji wasio kata tamaa.

“Alipoitwa kikosini kwa mara ya kwanza alivumilia kukosolewa sana. Alikuwa anasemwa sana vibaya kila kona. Rafiki pekee aliyemwamini ni jitihada zake binafsi.

Tutaendelea usikose makala ijayo

Shaffih Dauda (Instagram na facebook) kupata taarifa kabambe. Dauda Tv youtbe ndio kila kitu. Mimi ni Privaldinho (instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here