Home Ligi EPL Uhusiano wa Paul Pogba na United wazidi kupasuka, anataka kuondoka

Uhusiano wa Paul Pogba na United wazidi kupasuka, anataka kuondoka

15162
0

Waswahili wanasema lisemwalo lipo na kama halipo linakuja, lakini lisemwalo kuhusu Paul Pogba na Manchester United inaonekana sasa limewadia na hali si hali Old Traford.

Siku ya leo magazeti mengi ya nchini Uingereza yameibuka na taarifa kwamba Paul Pogba anataka kuondoka na hajali nini kitatokea ila yuko tayari kulazimisha uhamisho huo utokee.

Pogba haswa amekuwa akiota kuichezea Barcelona na taarifa zinasema kwamba hata kwenda United haikuwa matakwa yake makuu, bali alitamani tangu mwanzo kwenda Barcelona au Real Madrid.

Katika mchezo wa kwanza wa United katika EPL hapo majuzi dhidi ya Leicester Paul Pogba alipewa kitambaa cha unahodha ili kujaribu kumshawishi kuendelea kuitumikia United.

Lakini baada ya mechi hiyo kuisha Pogba alinukuliwa akisema hawezi kuongelea nini mustakabali wake United kwani lolote atakalosema anaweza kupigwa faini.

Inadaiwa kwamba baada ya Pogba kutoa kauli hiyo, kocha Jose Mourinho amekasirika sana na kushtushwa na maneno ya Pogba na Ijumaa wiki hii anaweza kuongelea hali ya Pogba na United kwa sasa.

Mourinho ndio sababu kubwa ya Pogba kutaka kuondoka.

Kuna muunganiko wa sababu nyingi zinazotaka kumuondoa Paul Pogba Manchester United lakini sababu kubwa zaidi ni kocha wa Manchester United Jose Mourinho.

Mourinho amekuwa akivutana na Pogba kuanzia uwanjani ambapo Paul huwa hafurahishwi na mbinu za Jose Mourinho ndani ya uwanja haswa za kujilinda na anatamani acheze kama alivyokuwa akicheza Juventus.

Kulikuwa na tetesi kwamba Pogba ameshawaambia baadhi ya wachezaji wenzake kwamba dili lake na Barcelona liko poa na anatamani likamilike aanze kwenda kuitumikia klabu hiyo.

Mwezi wa tisa mwaka jana Pogba alipata majeraha katika mechi dhidi ya Fc Basle, lakini wakati Mourinho akitumia timu ya wauguzi wa United kumshauri Pogba, nyota huyo aliamua kuajiri muuguzi wake binafsi suala ambalo Jose alikasirishwa nalo.

Mbaya zaidi kuna habari zinasema baada ya Mourinho kumuambia Pogba kwamba kama anataka kuongelea uhamisho amfuate yeye lakini Pogba alimjibu Jose Mourinho na kumuambia kwamba kauli kama hizo akamuambie Mino Raiola wakala wake

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here