Home Kitaifa Ufafanuzi wa Yanga kuhusu mchezaji Gustapha Saimon

Ufafanuzi wa Yanga kuhusu mchezaji Gustapha Saimon

4045
0

Kaimu Mwenyekiti wa Yanga Samuel Lukumay amefafanua uhalali wa Yanga kumtumia mchezaji Gustapha Saimon ambaye analalamikiwa na Singida United kwamba ni mchezaji wa Dar City ya ligi daraja la kwanza lakini Yanga ilimtumia mchezaji huyo dhidi ya Singida United kwenye mchezo wa ligi kuu.

Lukumay amesema Yanga imemtoa Gustapha kwenye kituo cha KISA ambacho kinalea na kukuza vipaji vya soka na taratibu zote zilifuatwa.

“Mchezaji huyo alikuwa na mgogoro na timu ya Dar City na tumekuwa naye kwenye timu yetu ya vijana na kuonesha uwezo mkubwa lakini hatukuweza kumtumia kwenye mzunguko wa kwanza kwa sababu alikuwa na mgogoro na timu yake ya awali.”

“Mwisho wa siku sakata hilo (mgogoro) lilifika TFF na baada ya kujiridhisha mchezaji huyo ni halali wa Dar City wakatupa idhaini ya kumtumia kwa hiyo ni mchezaji wetu halali ambaye tumeanza kumtumia katika mzunguko huu wa pili baada ya sakata lake lililokuwa na shauri TFF kumalizika na tukapewa lesni ya kumtumia.”

“Hatufahamu kwa undani lakini mchezaji huyo kuna academy ambayo ilikuwa inammiliki na wakampeleka Dar City kwa mkopo wamtumie kwa muda na baada ya muda kuisha mchezaji akawa huru sisi tukamchukua kwenye timu yetu ya U20 tulipoona anauwezo tukampandisha.”

“Tulipofika TFF tukaambiwa hatuwezi kupata leseni kwa sababu mchezaji huyo ana mgogoro na timu yake ya kwanza baadaya mgogoro huo kufika mwisho, wakaidhinisha kwamba sisi tupewe leseni ya kumtumia.”

“Kwa hiyo Gustapha ana baraka zote za TFF baada ya mgogoro wake na timu yake ya zamani kufikia kikomo.”

“Gustapha yupo kwenye timu yetu ya vijana kwa muda mrefu, tumemchukua kwenye academy aliyokuwa anaitumikia baada ya kumaliza muda wa kuitumikia Dar City.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here