Home Ligi LA LIGA Uchambuzi kuelekea mchezo wa Real Madrid vs Valencia

Uchambuzi kuelekea mchezo wa Real Madrid vs Valencia

5514
0

Mechi: Real Madrid vs Valencia

Mahali: Dimba la Estadio Santiago Bernabeu,

Muda: majira ya saa 22:45 usiku.


Real Madrid

Katika michezo 10 dhidi ya Valencia, katika ligi kuu katika uwanja wa Bernabeu ameshinda mara 5 sare 5 pia katika michezo 7 ya mwisho wametoa sare michezo 5.

Valencia

Wameshindwa kupata ushindi dhidi ya Real Madrid, katika dimba la Santiago Bernabeu, kwenye ligi kuu mara ya mwisho kumfunga Real Madrid,ilikuwa mwaka 2008, chini ya Ronald Koeman, kwa mabao 3-2.

Real Madrid

Valencia ni moja ya timu zilizofungwa zaidi la liga pale Bernabeu. Wamemfunga Espanyol, mara 67 katika uwanja wa nyumbani kwenye ligi kuu halafu anayefuatia ni Valencia, aliyemfunga mara 60 kwenye historia.

Valencia

Ndiyo timu iliyotoa sare mara nyingi zaidi dhidi ya Real Madrid, katika dimba la Bernabeu, katika michezo 10 ya mwisho wametoa sare mara 5.

Real Madrid

Wamekusanya alama 20 kwenye la liga msimu huu.

Ushindi mechi 6, sare 2 na amepoteza mara 5. Hii ni rekodi yao mbovu tokea msimu wa mwaka 2001/02 ambapo walivuna alama 19 kwenye mechi 13 za awali.

Gareth Bale ameshindwa kufunga bao katika michezo 9 ya ligi kuu pia amecheza dakika 731 bila ya kufunga bao hiyo ndo rekodi yake mbovu zaidi.

Shida nyingine ipo kwa mlinda mlango wa Real Thibaut Courtois ambaye amekuwa msimu mbovu. Mchezo wa mwisho dhidi ya Eibar

– kikosi cha Eibar: £48.27

– Thibaut Courtois: £58.50

Na Eibar walipata bao 3 dhidi ya Real Madrid. Mpaka kufikia sasa Coirtois amesharuhusu mabao 18 la liga. Je Navas arudi mzigoni au Thibaut aendelee kuvumiliwa.

Na Azizi Mtambo 15.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here