Home Kitaifa Ubora wa KMC unaanzia kwa kocha!

Ubora wa KMC unaanzia kwa kocha!

3519
0

Ubora na ushindani wa KMC unaanzia kwa kocha wa timu hiyo Ettiene Ndayiragije raia wa Burundi ambaye anaiongoza timu yake vizuri licha ya kuwa ni ngeni kwenye ligi kuu Tanzania bara.

KMC kumchukua Etiene Ndayiragije ilikuwa ni usajili bora kwao, alivyokuwa Mbao alifanikiwa kufanya iwe timu ya ushindani. Aliifikisha fainali ya kombe la TFF (Azam Sports Federation Cup).

Alizipa changamoto ya kutosha Simba na Yanga pale CCM Kirumba Mwanza na kuibakiza Mbao ligi kuu Tanzania bara. Msimu wake wa pili akiwa Mbao alijikuta kapoteza wachezaji wote wa kutegemewa kwenye kikosi cha kwanza (Salmin Hoza, Benedict Haule, Pius Buswita, Emanuel Mseja, Jamal Mwambeleko) akachukua vijana wapya wengine ambao hawakuwahi kucheza ligi kuu kabla na bado hakushuka daraja.

Ni kocha ambaye anajua anachokifanya, ameichukua KMC ikiwa ndio inacheza ligi kuu kwa mara ya kwanza kwenye histori watu wengi walitarajia ingekuwa bondeni inapambana lakini leo pamoja na Simba kuwa na viporo KMC ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 34 (ipo mbele ya Simba kwa mechi 8 zaidi).

Jana Ndayiragije aliiongoza KMC kushinda 5-2 dhidi ya Coastal Union ikiwa ni klabu pekee iliyopanda daraja msimu huu kushinda kwa idadi ya mabao 5 katika mechi mbili tofauti za ligi kuu hadi sasa kwa msimu huu (KMC 5-1 Tanzania Prisons, KMC 5-2 Coastal Union).

KMC imeshinda mechi nne (4) zilizopita mfululiozo, imefunga magoli 9 na kufungwa magoli mawili. Kaseja amepata clean sheets 3 katika mechi 4 za ligi zilizopita, ameruhusu magoli 2 katika dakika 360.

Inaelezwa kuwa, Etiene alichokifanya akiwa na Mbao katika msimu wake wa kwanza kwa kuifikisha fainali ya ASFC, KMC lengo lao ni kushinda ubingwa huo msimu huu ili kuiwakilisha Tanzania katika kombe la shirikisho Afrika msimu ujao.

Tuwaache KMC ‘wainjoi’ top 3 haijalishi hata kama ni kwa muda lakini tayari wamendika kwenye vitabu vyao wamewahi kukaa katika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi kuu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here