Home Kimataifa Tulikutana na kisiki”-Rais Simba

Tulikutana na kisiki”-Rais Simba

3843
0

Mwenyekiti wa klabu ya Simba Sweddy Mkwabi amesema benchi la ufundi litafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo wao dhidi ya AS Vita ili kuhakikisha wanafanya vyema katika michezo ijayo.

“Mimsingi kocha ameona makosa yaliyofanyika na atayafanyia kazi, tulikutana na strong timu AS Vita ni timu nzuri yenye wachezaji wenye uzoefu wengi ni national team level kwa hiyo tumekutana na kisiki kusema kweli, na sisi tulitengeneza nafasi lakini wachezaji wetu hawakuzitumia.”

“Bado tupo kwenye ligi hatujatoka kwenye mchezo hadi sasa hivi tuna pointi 3 na AS Vita wana pointi 3 na waoongoza ni Ahly wana pointi 4 kwa hiyo bado kundi letu lina ushindani tunaamini tunaweza kufanya vizuri.”

“Kama unakumbuka kuna wakati fulani TP Mazembe walichukua ubingwa wa Afrika lakini walifungwa goli 5 na Ismaily kwa hiyo lolote linawezekana.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here