Home Kitaifa Timu za Kenya zimetuzidi, tusitafute mchawi

Timu za Kenya zimetuzidi, tusitafute mchawi

3719
0

Timu mbili za Kenya (Bandari FC na Kariobangi Sharks) zimefuzu nusu fainali ya SportPesa Cup baada ya kushinda mechi zao dhidi ya timu za Tanzania (Singida United na Yanga).

Watu wengi wanajiuliza, timu za Bongo zinadharau haya mashindano au zinazidiwa uwezo na timu za Kenya?

Mimi nabaki kwenye uhalisia kwamba timu zetu zinazidiwa na timu za Kenya kwa sababu huu ni msimu wa tatu Tanzania tunaonekana wasindikizaji kwenye haya mashindano.

Misimu miwili iliyopita ilichezwa wakati ligi ya Tanzania imemalizika tukasingizia wachezaji wengi wanakuwa wameenda mapumzikoni, msimu huu mashindano yamekuja wakati ligi ipo katikati kwa hiyo hakuna sababu ya kunitetea.

Timu za Kenya katika level ya klabu zina ushindani mzuri, ligi yao inapangiliwa vizuri inawezekana ligi yao isiwe na pesa kama ilivyo ligi yetu lakini ni watu ambao wanaushindani halisi.

Zamani mashindano ya CECAFA inasemekana kuna namna ambavyo timu za nyumbani zilikuwa zinatengenezewa mazingira ya kufika mbali (hakuna uthibitisho) ili mashabiki waendelee kwenda uwanjani pesa ipatikane kwa ajili ya kukidhi baadhi ya gharama za uendeshaji.

Mashindano kama haya inaonekana waandaaji wamejipanga hawategemei mashabiki ili waendeshe mashindano, kila kitu kipo timu ambayo imejiandaa kushinda itashinda.

Baada ya kuona lineup ya Yanga na kuwaona Mrisho Ngasa, Haruna Moshi na Ibrahim Ajibu nikajua kuna shida tayari na ninavyozijua timu za Kenya zinacheza kwa nguvu sana kwa hiyo ili ucheze nao inatakiwa kila mchezaji atimize majukumu yake na mpira wa kileo sio wa kutegeana.

Mpira ukiwa kwa mpinzani inabidi muukimbize na ukiwa kwenu inabidi mkimbie sana kufungua nafasi ili kuendelea kucheza lakini kwa kile kikosi sikuona kama kile-balance ndio maana Kariobangi walikuwa strong halafu pia hata kwenye ligi yao tayari wamecheza mechi 8 bila kupoteza.

Kariobangi ni timu ngeni imeanzishwa mwaka 2000 ikapanda ligi kuu (KPL) mwaka 2017 ni watoto wa Nairobi ambao wanataka wacheze na wao waonekane. Niliona documentary ya golikipa wao anasema kwenye mashindano haya anataka acheze aonekane na wanajua kwetu kuna pesa kwa hiyo kuna wachezaji wamekuja na malengo.

Huwezi ukawa na Boban, Ngasa na Ajibu kwa wakati mmoja halafu ukapata matokeo mbele ya timu yenye ushindani kwa sababu wote hao wanaweza kucheza wakati timu inamiliki mpira, lakini mpira ukiwa kwa mpinzani hawawezi kupambana.

Hata mechi ambayo Yanga walifungwa na Stand, Boban, Ngasa na Ajibu walianza kwa pamoja huwezi kupata matokeo kwa style hiyo labda na timu zetu hizi za Bongo.

Unapowatumia wachezaji hao kwa pamoja lazima uwe una watu wa wanaoweza kufanya kazi kubwa wakati timu haina mpira, Ngasa na Boban tayari ni wakongwe na mpira wa kileo sio wa majina ni namna gani watu wanafanya kazi kiasi gani uwanjani na kujitoa kwa ajili ya timu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here