Home Kimataifa TBT: Fahamu kuhusu Bushman! Fedha zake zilibebwa na upepo

TBT: Fahamu kuhusu Bushman! Fedha zake zilibebwa na upepo

8403
0

Hivi unamkumbuka yule jamaa aliyecheza zile filamu ya Bushman? Hasa ile filamu ya “The Gods Must Be Crazy” unaambiwa alilipwa kiasi cha $300 ikiwa filamu iliingiza $60 milioni.NB: Bushman anayeonekana kwenye filamu ya Strike back ya 2010 sio yeye huyu. Yule wa Strike back anaitwa Andries Kruiper.
Huyu ni Andries Kruiper na sio aliyecheza filamu za Bushman

Coma alicheza kama muigizaji mkuu kweny“The Gods Must Be Crazy” lakini wazungu wakaamua kumlipa kiasi hicho cha fedha. Kama anavyoigiza kwenye filamu ni kweli ni mshamba maana maisha yake yote alizaliwa vijijini. Yale yalikuwa maisha yake halisi.

Picture Suggesting The Main Actor of 'The Gods Must Be Crazy' was Only Paid $300
The Main Actor of ‘The Gods Must Be Crazy’ was Only Paid $300

Chrispin Inambao alifanya nae mahojiano mwaka 2002 na kumweleza kuwa siku ya kwanza kupanda ndege alihisi kuchanganyikiwa.

“Ilikuwa kitu cha ajabu sana. Kila mara nilikuwa natazama nje. Nilikuwa na furaha lakini bado nilijawaha na uoga”

“Safari ya kwanza ilikuwa kwenye Afrika kusini kisha baadae Japan. Nilipofika Afrika kusini nilibaki nashaangaa tu miji. Ikikuwa jambo la ajabu kuwahi kuona majumba magari na miundo mbinu mingine”


Filamu yake ya kwanza alijulikana kama Xixo, alicheza kama kiongozi wa jamii ya watu wa Khoisan. Filamu yake ilivutia sana katika bara la Ulaya.

Katika filamu ya The Gods Must Be Crazy direkta Jamie Uys kutoka South African ndiye aliyemchagua acheze kama muigizaji mkuu.

Alikuwa haongei lugha yeyote rasmi, kama Kiingereza au Kiafrikaans.


Alicheza tena filamu ya Gods Must Be Crazy 2, mwaka 1990 ambayo alikuwa akimtafuta mwanae. Filamu hii ilimpa umaarufu mkubwa China na Japan.
Kampuni moja kutoka Hong Kong iliomba kufanya nae filamu nyingine Crazy Safari (1991), ambayo alicheza na Chinese vampire; filamu nyingine ni Crazy mwaka Hong Kong (1993) ambayo alikuwa akifukuzwa na watu mtaani wakimhisi kuwa alikuwa mwizi wa dhahabu. Filamu nyingine ni The Gods Must Be Funny in China, (1994), ambayo alicheza kama mtaalamu wa asili.
Miasha yake Namibia

Alizaliwa kule Tsumkwe nchini Namibia, N!xau Toma Hata hivyo pesa alizolipwa inasemekana zote zilipotelea mbali maana hakujua thamani ya fedha ni nini. Watafsiri wa mambo wanasema kuwa katika maisha yake kabla hajacheza filamu ya kwanza alibahatika katika maisha yake kuonana na wazungu watatu tu kabla ya waendeshaji wa filamu kumfikia.

Picture from 'The Gods Must Be Crazy' Movie

“Nilipewa kiasi cha fedha ambacho sikujua ni nini. Wakanipa elimu ya karatasi za fedha. Niliwaambia sihitaji lakini wao wakaniambia sitaweza kuishi bila karatasi zile. Niliwacheka sana. Mababu zangu wameishi miaka mingi bila hizo karatasi leo wananiambia sitaweza kuishi kivipi”


Inasemekana baadae aligundua thamani ya fedhia miaka ya 1990s. Miaka hiyo alizitaka kampuni zilizomfuata kucheza nae filamu zimlipe maelfu ya dola kabla ya kurudia filamu yake ya pili. Alipulizwa kuhusu fedha hizo atazifanyia nini aliwajibu

“Kijijini kwetu hakuna maji, hakuna Umeme, tunaishi kwenye nyumba za nyasi. Nataka nikaweke umeme na kuchimba kisima cha maji

Gcao Coma baadae aliporudi Namibia alipewa tuzo ya golden handshake yenye thamani ya N$150 000 (ambayo ni sawa na Tsh Milioni 22,500,000) kutoka kwa kampuni ya Mimosa Films kama tuzo ya heshima.

Coma anasema miaka ya nyumba alitengeneza nyumba yenye thamani ya N$ 80 000, sawa na milioni 12,000,000 Milioni za kitanzania miaka ya 1980.

Gcao Coma alitumia N$ 15000 kununua gari (used) aina ya Chevrolet na kumwajiri dereva aliyekuwa akimlipa N$150.


Kwa kuwa maisha yao yalikuwa ya uwindaji alijaribu pia kufanya ufugaji ambapo alinunua ng’omne 15 kwa thamani ya N$600 kila mmoja sawa na 90,000 za Tz kwa ng’ombe mmoja na kununua mbuzi 15 na mbuzi mmoja alikuwa na thamani ya N$50.

Picture from 'The Gods Must Be Crazy' Movie

Jambo la kuchekesha ni kwamba Gcao Coma anadai ng’ombe walipokuwa wanaongezeka ilibidi wengine awauze au atoe zawadi kwa watu kwa sababu alikuwa anashindwa kuwahesabu. Yeye alikuwa na uwezo wa kuhesabu moja mpaka ishirini tu. Hivyo alikuwa anaogopa kuwapoteza na wangeibiwa bila yeye kujua. Tehe tehe tehe.

“Nilikuwa nataka ng’ombe 10 tu. Baadae nilijitahidi wakafika 15. Sikuweza kuendelea kuhesabu. Baadae nikagundua ng’ombe wangu 8 waliliwa na Simba. Hivyo nikagundua nilikuwa napoteza ng’ombe wengi bila kujua”


Gcao Coma mwaka 1980, alipewa dola 300 sawa N$3000 alipokuwa akicheza filamu yake ya awali.

Akiwa nyumbani kwake pia aliwahi kusahau saa yake ya gharama kubwa kabisa aina ya Rolex ambayo iligharimu takribani milion 3 za kitanzania kwenye kichaka alipokwenda kuokota matunda maarufu kama makwevo kwa lugha ya kirukavango. Coma alipofika nyumbani akakumbuka kuwa aliacha saa yake mbali. Lakini hakwenda kuitafuta maana kwanza hakuona thamani ya hiyo saa ila aliona inamkera tu mkononi.


Alipokuwa akimaliza kuigiza filamu alikuwa anaitazamani sehemu ya kutengenezea filamu lakini ndugu zake wengine hawakuwahi kuziona filamu hizo. Alipewa tepu ya filamu aliiuza kwa askari mmoja kiasi cha N$ 50 kwa sababu hakuwa na sehemu ya kuipeleka.

Gcao Coma aliwajengea ndugu zake wote nyumba za kuishi na kuwasaidia kwa mambo yote ya kijamii. Tokea mwaka 2000, Gcao Coma alikuwa akipokea kiasi cha N$2 000 sawa na 300,000 za kitanzania kila mwezi kama malipo ya pensheni kutoka kwa makampuni ya filamu aliyowahi kufanya nayo kazi.


N!xau baada ya kuzurura ulaya na Asia kwa takribani miaka 10 ni kweli alijihusisha na maisha ya kisasa lakini mwenye asili haachi asili yake baadae aliamua kurudi kwenye nyumba yake huko Kalahari


Picture of N!xau Toma
N!xau Toma

Inasemekana kuwa N!xau alifariki dunia nje kidogo ya nyumba yake kwa Ugonjwa wa TB alipokuwa akiokota kuni katikati mwa jangwa la Kalahari. Taarifa zinasema haikuwa inajulikana ni upi umri wake sahihi lakini inakadiriwa kufikia miaka 59.

Mpaka anakufa alisema anatamani sana kuendelea kucheza filamu yeyote kwani ni kipindi kirefu hajapata fursa hiyo tena.

N!xau (1944–2003)


N!xau Picture

Makala na Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here