Home Kimataifa Tathmini fupi ya mchezo wa Arsenal vs United

Tathmini fupi ya mchezo wa Arsenal vs United

3991
0

Mchezo wa ligi kuu England uliyomalozika muda mchache Arsenal, akiwa nyumbani kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Manchester United.
.
.
Arsenal, walikuwa bora zaidi kwenye idara ya kiungo kuliko Manchester United.
.
.
Kochacwa klabu ya Arsenal, Unai Emery, aliamini kabla ya hii mechi kuwa Wapinzani wake Manchester United, watakuwa bora kwenye idara ya kiungo kutokana na hata michezo yao ya nyuma walichocheza ukiwemo ule mchezo dhidi ya Paris Saint Germain.
.
.
Unai,leo alitegeneneza mfumo wa kumzunguka Paul Pogba, mbele ya viungo wake wawili wakabaji Aron Ramsey,na Xhaka walikuwa walikuwa wanamfanyia press Pogba, akishika mpira na kujikuta akipoteza mpira mbele ya viungo wa Arsenal.
.
.
Pogba ni moja ya viungo wenye hatari duniani akiwa na mpira kama huna maamuzi ya haraka ana uwezo wa kuanzisha mashambulizi na hata kupiga pasi za mwisho muda mwingi leo alinyimwa uhuru mpaka dakika 90 alipiga pasi moja tu yenye madhara kwa mpira mrefu na kumkuta Lukaku.
.
.
Ramsey, na Xhaka, leo wefanya kazi kubwa sana walikuwa na uwezo wa kuzunguka katika eneo hilo na kutibua mipango ya Pogba.
.
.
Fred,Matic, leo hawakuwa na kwenye kiwango bora sina Mashaka na Matic,kwa maana katoka majeraha.
.
.
Fred, amekuwa akipoteza mpira kwenye idara ya kiungo leo kacheza ovyo sana tofauti na mchezo dhidi ya Paris Saint German.
.
.
Ashley Young, umri umeenda sana amekuwa akipoteza mpira sana na upande wake watu wamekuwa wakipita sana hivi kwa nini?namba ya kudumu Asichukue Dalot , moja ya beki mzuri wa pembeni wanaokuja kwa sana.
.
.
By Azizi Mtambo 1

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here