Home Kimataifa Takwimu za Man United vs Burnley

Takwimu za Man United vs Burnley

2940
0

Manchester United Vs Burnley, mchezo huu utapigwa majira ya saa 23:00 kamili usiku katika dimba la Old Trafford.


…………..Toka walivopoteza mchezo wa Kwanza kwenye ligi kuu England dhidi ya Burnley, mnamo mwezi August, 2009 Manchester United, hajapoteza mchezo hata moja kati ya michezo 8 dhidi ya Burnley, ameshinda mara 5 na sare mara 3 pia amepata clean sheet sita kwenye michezo hiyo………….Burnley, hajashinda mchezo hata moja kati ya michezo 19 dhidi ya Manchester United, katika michuano yote amepoteza mara 12 na sare mara 7 toka mara ya mwisho kupata ushindi ilikuwa mwaka 1962 kwa mabao 5-2.…………Manchester United, ndo timu yenye wastani mkubwa kushinda michezo inayochezeka siku ya Jumanne, ana wastani wa asilimia 62.5 kuliko timu yoyote kwenye ligi kuu ameshinda michezo 30 kati ya michezo 48………….Pia kocha wa klabu ya Burnley, ndo kocha ambaye amecheza michezo mitano siku ya Jumanne, kwenye ligi kuu England hajapoteza hata moja ameshinda mara 3 na sare 2………….Toka Burnley, alivomfunga Chelsea, kwenye mchezo wa ligi kuu wa ufunguzi msimu wa mwaka 2017-18 Burnley, hajashinda mchezo hata moja katika michezo 8 ya ugenini dhidi ya vilabu vikubwa sita vya juu pia amepoteza michezo minne mfululizo kwa kuruhusu mabao 14.…………Ole Gunnar, kama atashinda mchezo wa leo atakuwa kocha wa Kwanza katika ligi kuu England kushinda michezo 7 Carlo Ancelloti (Chelsea), na Pep Guardiola(Manchester city) wote hao wameshinda michezo sita………….Romelo Lukaku, amehusika kwenye upatikanaji wa mabao sita katika michezo sita dhidi ya Burnley, aliyocheza amefunga mabao 4 na assist 2.…………Marcus Rashford, amefunga katika michezo minne ya mwisho kwenye ligi kuu England akiwa na Manchester United, na kama atafunga leo atakuwa mchezaji wa tatu mwenye umri mdogo kufunga katika michezo mitano mfululizo kwenye ligi Kuu nyuma ya Nicholaus Anelka, mwaka 1998, na Jose Antonio Reyes, mwaka 2004.By Azizi_Mtambo 15

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here