Home Kimataifa Takwimu kuelekea mtanange wa Arsenal na Man United

Takwimu kuelekea mtanange wa Arsenal na Man United

4517
0

Fa Cup- Raundi ya nne

Mchezo huu utaanza saa 4:55 usiku, kwa saa za Afrika Mashariki.


Takwimu za mchezo wenyewe.

Arsenal

Arsenal wameshinda mechi mbili zilizopita za Fa Cup nyumbani kwa Man United

Hata hivyo, Arsenal wameshinda mechi moja kati ya sita walizokutana na Man United kwenye mashindano yote( sare 2, kupoteza 3)

Kumekuwa na kadi nyekundu tano katika timu hizi mbili.

Arsenal wamepoteza mechi mbili za nyumbani kwenye mashindano yote msimu huu, wakishinda 13 na kutoa sare 3

Wamefika raundi ya tano mara saba katika misimu nane iliyopita, ni mara moja tu wameshindwa kufanya hivyo, walipokutana na Nottingham Forest msimu uliopita.

Mechi ambazo Arsenal wameitoa Man Utd kwenye Fa Cup, wameenda moja kwa moja kucheza Fainali na kuchukua ubingwa- msimu wa 2002- 2003, 2004, 2005 na 2014-2015

Man United

Man United wameshinda mechi zote saba chini ya Ole Gunnar Solskjaer, wakifunga magoli 19 na kuruhusu mengine manne.

Wameruhusu goli moja katika mechi tatu za ugenini tangu Solskjaer alipoichukua timu hiyo

Manchester United wamepoteza mechi moja kati ya 14 za fa Cup kwenye raundi ya 4

Romelu Lukaku amefunga magoli 13 kwenye mechi zake 14 zilizopita, ukijumuisha mara sita kwenye mechi saba za United.

Akiwa na magoli tisa na assist 9, Alexis Sanchez amehusika kwenye magoli 18 katika Fa Cup kipindi akiwa Arsenal na sasa akiwa Man United.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here