Home Kimataifa Takwimu kuelekea kivumbi cha Chelsea vs City

Takwimu kuelekea kivumbi cha Chelsea vs City

3910
0

Man city Vs Chelsea: Uchambuzi kuelekea mechi kati ya Man City Vs Chelsea, ambayo itaanza saa 1:00 Usiku.


Je, Pep Guadiola atakubali kufungwa tena na Chelsea mara bili ndani ya msimu mmoja?


Hii itakuwa ngumu sana. Mechi ambayo Chelsea alishinda 2-0, kwenye uwanja wa Stamford Bridge, Raheem Sterling alilazimika acheze namba 9 kwasababu ya kukosekana kwa Sergio Aguero.Leo Aguero yupo. Nafikiri kama City watatengeneza nafasi nyingi Aguero lazima azitumie vizuri. Mechi ya kwanza walitengeneza nafasi nyingi kipindi cha kwanza lakini hawakuzitumia kwa ufasaha.Pep atakuja tofauti leo, Kyler Walker na Laporte watawasaidia Sterling na Sane kuipeleka timu mbele.Pia Kelvin Debruyne na Fernandinho watahitaji kutumia njia nyingine ya kupiga mipira mirefu kwa Sterling na Sane, endapo Chelsea watakuwa wanabana uwanja.Naamini Chelsea hawataweza kuwafanya Man City wasikae na mpira dakika zote 90. Kumfanya mpinzani wako asifurahie umiliki wa mpira dakika zote 90, inahitaji uwe na mapafu ya mbwa.Kuna muda Chelsea watachia tu. Baadhi ya wachezaji wa Chelsea watapumua kidogo kufanya (pressing) Ule muda ndio Man City watakuwa makini zaidi katika kutumia nafasi, na kwakuwa Aguero yupo, bila shaka hatawaangusha.Kwa upande wa Chelsea, Maurizio Sarri, anajua kabisa magoli waliyofunga kwenye mechi ya awali, haikuwa rahisi. Walifunga kwenye mazingira magumu.Atakachowambia wachezaji wake, ni kupokonya mpira mara wanapoupoteza.Inahitaji kufanya mazoezi na sio kujaribu wakati wa mechi husika. Chelsea wakiwa wanashambulia, wanatumia mfumo wao wa 4-3-3. Ila wakiwa hawana mpira hasa wanapocheza na City lazima wabadilike na kufanya mfumo uwe 4-5-1 kwasababu ya kukaba nafasi na kubana uwanja pia.Kuwakabili Man City lazima ukabe nafasi, usiwaalike wafike kwenye eneo lako la ulinzi. Ukimfata mchezaji mmojammoja, wanakuadhibu maana unakuwa unaacha nafasi nyuma.Chelsea watawategea Man City wafike mpaka katikati ya uwanja ili watengeneze umoja wa kuzuia kama walivyofanya mechi ya kwaza.David Luiz, ataanzisha mashambulizi na hata kupiga mipira mirefu kwa Pedro au Willian kipindi City hawana mpira.Kazi nyingine itakuwa kwa Cezar Azipilicueta na Alonso.Upande wa Alonso huwa kuna shida kidogo sababu ni mzuri wakati anashambulia. Sitegemei mabeki wa pembeni wa Chelsea kushambulia sana.Kupaki basi, kukaba na kuhakikisha hakuna nafasi inayowaruhusu City kupenya itakuwa msaada kwao.Admila Patrick

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here