Home Ligi EPL Taarifa kuelekea mtanange wa Arsenal vs Spurs

Taarifa kuelekea mtanange wa Arsenal vs Spurs

6055
0

Na Patrick Admila

Hapo kesho siku ya Jumapili, kutakuwa na mchezo wa patashika nguo kuchanika wa Ligi Kuu ya Uingereza, utakaowakutanisha wababe kutoka Kaskazini mwa Jiji la London Arsenal dhidi ya Spurs


Mtanange huu utaanza majira ya saa 11:05 jioni, kwa saa za Afrika Mashariki.


Vilabu vyote viwili viko kwenye kiwango kizuri.

Tottenham wameshinda mechi zao tatu zilizopita za ligi kuu ya Uingereza, na Arsenal hawajafungwa kwenye mechi zao 11 za Ligi kuu ya Uingereza. Ujio wa Mwalim Emery Unai umefufua matumaini makubwa ya washika mitutu hao wa London.

Kwa upande wa Spurs nao wameonesha ukomavu wa hali ya juu ndani ya wiki moja baada ya kutoa kichapo kwa mahasimu wao wakubwa Chelsea ambao walikuwa wakishikilisa rekodi ya kutokupoteza mchezo hata mmoja msimu. Katika ya wiki pia Spurs wakatoa dozi ya bao 1 kwa bila kwa Inter Milani kwenye michuano ya klabu bingwa.

Najua macho ya watu wengi yatakuwa kwa washambuliaji wawili, Pierre Aubemeyang na Harry Kane. Lakini umakini unatakiwa kuwepo kwa viungo wabunifu wawili ambao ndio msaada mkubwa kwa washambuliaji hao wawili. Kwa namna moja au nyingine ni wachezaji wanaoweza kuamua mechi husika. Makocha wa timu zao wanatengeza mfumo kuwazunguka wachezaji hao, ambao ni Ozil na Christian Ericksen. Ozil akiwa kwenye ubora wake, ukiruhusu ainue macho juu, basi umekwisha. Sawa na Ericksen pia.

Ni swali gumu sana kuamua nani bora kati ya Ozil na Ericksen, kwasababu ni wachezaji wa aina moja. Ukitaka kuamini angalia wote karibu wanakaribiana kwenye takwimu zao. Lakini Ericksen anaonekana ni kiungo aliyekamilika kuliko Ozil. Ericksen anatengeneza nafasi nyingi zaid, anafunga zaidi na anachangia pia magoli ya Tottenham kwa pamoja. Pia Ericksen anaweza kuongeza mchango wa ulinzi kwa timu yake ikiwa haina mpira. Ericksen amemzuia adui mara 227, wakati Ozil amefanya hivyo mara 140 kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.

Ozil amekuwa akikosolewa kwa misimu kadhaa iliyopita. Wengine wamekuwa wakimuona dhaifu au mzembe hasa pale mechi inapokuwa inahitaji kucheza kimbinu zaidi. Kitu kingine kinachomrudisha Ozil nyuma, ni muendelezo wa kiwango chake kila msimu. Maana amekuwa hachezi mechi za Arsenal mara kwa mara. Wakati Ericksen yeye amekuwa kama mtu muhimu kwa Spurs.

Ukitaka Spurs isitengeneze mashambulizi, hakikisha viungo wako wanamfanya Ericksen awe na siku mbaya ofisini. Sawa na na Ozil pia. Kocha Maurisio Potchetino wa Spurs, hata mechi ikiwa inahitaji kucheza kwa nidhamu ya hali juu hawezi kumtoa Ericksen mchezoni kwasababu kila anachoagizwa afanye anatekeleza tofauti na Ozili ambaye muda mwingine Kocha Unai emery anasema, kuna wakati anamuacha nje Ozil kwasababu mechi zingine zinahitaji ucheze kwa kutumia nguvu.

Kitu kingine kinachombeba Ozil mpaka sasa ni staili yake ya uchezaji na ni kipenzi cha mashabiki kuliko Ericksen
:
:
:
Pamoja na hayo yote, Ozil akiwa kwenye ubora wake ule tunaoujua naamin unaweza kusema Ericken kwa Ozil bado, kwasababu Ozil amekuwa na mapungufu kama nilivyosema kabla, ndomaana unaona kiwango chake hakionekani kila wiki.

Tukutane Jumapili jioni

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here