Home Kimataifa Suarez ni usajili sahihi kwa Arsenal

Suarez ni usajili sahihi kwa Arsenal

5779
0

Klabu ya Arsenal, imekamilisha usajili wa Kiungo wa klabu ya Barcelona, Denis Suarez, kwa mkopo akitokea klabu ya Barcelona.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 mkataba wake na klabu ya Barcelona, unafikia tamati mnamo mwaka 2021.

Kiungo huyo ambaye alianza kuitumikia timu ya wakubwa mwaka 2016 tayari mpaka sasa ameichezea Barcelona, michezo 71 na amefunga mabao 8 na kutwaa mataji 5.

Suarez alikosa nafasi ya kudumu ndani ya Barca.

Mara kadhaa alikuwa akitolewa kwa mkopo kwa vilabu mbalimbali. Huu ni wakati wa yeye kuonesha kuwa ana uwezo mkubwa. Arsenal imempoteza Ramsey na Ozil ameyumba kimahusiano na mwalimu wake.

Kinda huyu ana kila sababu ya kupata nafasi klabuni Arsenal ili kuonesha makali yake. Ni matarajio yangu kuwa hatabakia Arsenal.

Barcelona wamejaa wachezaji wengi sana wenye uwezo na uzoefu kumzidi yeye ndio maana amekuwa haaminiki hata kidogo. Ujio wa Athur Mello kumeondoa kabisa uwezekano wa kijana huyu kupata nafasi.

Hivyo wamempeleka huku kwa Unai anoe makali yake. Kiwango chake ndicho kitakachotoa mwelekeo wa aidha kuuzwa kwake au kurudi kama ilivyokuwa kwa Fabregasi na Pique.


Tottenham wanakuwa klabu ya kwanza kuwahi kutokea katika Historia ya Ligi kuu ya Uingereza kutofanya usajili wowote ule katika madirisha mawili ya usajili mfululizo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here