Home Dauda TV Story yenye huzuni na matumaini, uvumilivu umemkutanisha Hazard na Jokate hatimaye ndoto...

Story yenye huzuni na matumaini, uvumilivu umemkutanisha Hazard na Jokate hatimaye ndoto zinatimia

18108
0

Siku zote usikate tamaa kwenye maisha kufanikisha kile ambacho unakiamini, haijalishi utapita kwenye changamoto zipi, itakuchukua muda kiasi gani kufikia malengo lakini pambana kwa kile unacho kiamini hadi ukifanikishe.

Kwa nini nasema hivyo?  Juzi kati hapa nilikuta na mrembo Jokate Mwegelo akanisimulia story hukusu kijana mmoja anajulikana kwa jina la Hazard Ibrahim ambaye anapambana kuifikia ndoto zake.

Kijana huyo anacheza mpira wa miguu kwa hiyo moja kwa moja Jokate akaamini akinikutanisha na bwana mdogo naweza kumsaidia kwa namna moja au nyingine kwa kuwa jambo hilo lipo katika sekta yangu.

Historia ya kijana huyu inasikitisha lakini mwisho wa siku imejaa matumaini, Hazard anaishi na mama yake maeneo ya Ilala Bungoni, baba yake alifariki muda mrefu. Familia yao inamtegemea mama, wanaishi na kusoma kwa mgongo wa mama yao ambaye anajishughulisha na biashara ya kuuza chai na vitafunwa.

Hazard alikutanaje na Jokate?

Mwaka juzi Jokate alialikwa kama mgeni rasmi kwenye mahafali ya kidato cha nne kwenye shule ya sekondari Majani ya Chai, Hazard alitangazwa mwanamichezo bora hivyo akakabidhiwa zawadi (tuzo) yake na Jokate. Hii ilikuwa ni fursa kwa kijana Hazard na aliamini atatimiza malengo yake kupitia Jakate ambaye atakuwa daraja la yeye kufika mahali anapotaka.

Baada ya muda akaanza harakati za kumtafuta Jokate ili kumweleza juu ya kipaji chake na kuomba msaada asaidiwe kufikia malengo. Hakuwa na namba ya simu wala hakujua atakutana wapi tena Jokate hivyo haikuwa kazi rahisi kwake, ndipo alipoamua kutmia mtandao wa Instagram kufikisha ujumbe wake.

Alikuwa akimtumia sms nyingi DM lakini kutokana na harakati na majumu mengi Jokate alikua hajawahi kupitia ujumbe ambao amekuwa akitumiwa na Hazard. Kijana hakukata tamaa kwa sababu aliamini ipo siku atafanikiwa akawa anamtumia picha zake akiwa mazoezini na kumkumbusha anahitaji kusaidiwa ili kufikia ndoto zake.

Dili linatiki

Kila ifikapo Machi 20 ya kila mwaka Jokate Mwegelo huadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwake (birthday), Machi 20 mwaka huu (2018) Hazard alipost picha ambayo alikuwa akipokea tuzo ya mchezaji bora aliyokabidhiwa na Jokate miaka miwili liyopita kisha akam-tag Jokate. Kama haitoshi akamtumia Jokate picha hiyo DM na kumkumbusha historia ya picha hiyo na kile ambacho anahitaji kwa sasa kutoka kwa mlimbwende huyo.

Katika peruziperuzi za Jokate kwenye simu yake akakumbana na sms na picha za Hazard, zilikuwa nyingi na zinaelezea lengo lake la kutaka kufika mbali katika career yake ya soka. Jambo jema ni kwamba katika sms ambazo Hazard alikuwa amemtumia Jokate aliwahi kutuma na namba yake ya simu ya mkononi kwa hiyo Jokate alimpigia simu wakazungumza mengi na kumuahidi atakwenda nyumbani kwao kumtembelea na kuona namna ya kumsaidia.

Nyumbani kwao hazard

April 8, 2018 Shaffi Dauda na Jokate waliongozana mpaka ilala bungoni kwenda kukutana na kijana Hazard, waliongea mambo mengi, Shaffih akakubali kumjumuisha Hazard kwenye kampuni yake ya Shadaka Sports Management hivyo anaungana na wachezaji wengine ambao wapo chini ya kampuni hiyo inayosimamia wanamichezo mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.

Darasa alilotoa Hazard kwa vijana wengine

Namna Hazard alivyoweza kujipambanua kwa ujasiri na kuamini lengo lake litafanikiwa bila kujali litachelewa kiasi gani. Uvumilivu wake umemlipa, licha ya kutuma sms na picha kwa Jokate bila majibu bado hakukata tamaa na kuishia njiani aliamini ipo siku, kwa hiyo hupaswi kukata tamaa na kuishia njiani kwa kile unachoamini kuna siku utafanikiwa kupitia hicho.

Bidii yake katika kutafuta mafanikio licha ya mazingira kumrudisha nyuma lakini anaamini yeye ni zaidi ya mazingira yake na atashinda.

Uwezo wake wa kutumia mitandao ya kijamii kwa manufaa, licha ya kuwa na umri mdogo ameweza kutumia mitandao vizuri kama chombo cha kumsaidia kufikia mafanikio yake.

Video ya kwanza Jokate akimsimulia Shaffih Dauda kuhusu kijana Hazard na kumshawishi wakutane naye

Video ya pili Jokate na Shaffih nyumbani kwao hazard na walivyopanga kumsaidia afikie ndoto zake

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here