Home Ligi EPL Son Heung Min kupelekwa jeshi baada ya kufeli timu ya taifa, hii...

Son Heung Min kupelekwa jeshi baada ya kufeli timu ya taifa, hii sheria vipi Bongo?

12902
0

South Korea hakuna ulelemama, kama wewe ni kijana ambaye hujafikisha miaka 28 na huna tatizo lolote la kiafya baasi ni lazima uende jeshini ukalitumikie kwa muda wa miaka miwili.

Mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Hotspur Son Heung Min anakaribia naye kwenda kujiunga na jeshi la nchini humo mapema mwakani.

Msimu wa 2018/2019 unaweza kuwa wa mwisho kwa striker huyu na baada ya hapo atakwenda jeshini, lakini Heung Min anaweza akalikwepa hili la jeshi kama kuna jambo atalifanyia taifa lake.

Hii inamaanisha kwamba kama anaweza kuisaidia timu yao ya taifa kufanya vizuri mwaka 2019 katika michezo ya Asia baasi hatakwenda jeshini atasamehewa.

Mwanzo Son na wenzake walipewa nafasi kuikwepa adha hiyo ya kutokwenda jeshini kupitia kombe la dunia lakini matokeo mabovu yaliwafanya kuendelea kusubiria kwenda jeshi.

Kwa Korea Kusini kama ukikataa kwenda jeshi katika miaka hiyo miwili kinachotokea ni jela, zaidi ya raia 400 nchini Korea wanatumikia kifungo gerezani baada ya kukataa kwenda jeshini.

Kama unakumbuka nyota wa zamani wa Leicester City Ki Sung Yeung aliambiwa arudi kwao siku ya mechi vs Man City ili kuanza kulitumikia jeshi baada ya kutofanya lolote. kubwa katika michezo.

Unadhani kwa matokeo mabovu tuliyonayo Watanzania katika soka, kama sheria hii ikija Tanzania nani atapona?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here