Home Kimataifa Skendo ya Giggs kumsaliti mke wa kaka yake yaitesa familia

Skendo ya Giggs kumsaliti mke wa kaka yake yaitesa familia

4596
0

Kaka yake Ryan Giggs bwana Rodri Giggs amesema kama mdogo wake (Ryan) atamtafuta hana tatizo na hilo.

Kwa kipindi kirefu familia ya Giggs imekosa ushirikiano mara baada ya skendo ile.

Hii ni mara baada ya ndugu hao kuishi miaka 7 bila mawasiliano.

Ryan Giggs nyota wa zamani wa klabu ya Man United alikumbwa na kashfa ya kutembea na mke wa Rodri bibie Natasha miaka 8 iliyopita.

Hata hivyo Miezi 2 baada ya kashfa ile Giggs alimuomba Rodr Msamaha lakini mawasiliano yakavunjika baina yao.

Rodri aliachana na mke wake pia Ryan aliachana na mkewe Stacey.

Rodri analalamika kuwa kaka yake alikuwa mkweli lakini akishindwa kutimiza ahadi. Kuna taarifa zinadai kuwa bado wawili hao waliendelea na mahusiano ya siri mara baada ya tukio lile.

Giggs kwa sasa ni kocha wa Wales na mara kadhaa amekuwa mkimya sana kuongelea tukio hilo ambalo lilichafua sana jina lake.

Rodri alipoulizwa jana kama anaweza kuongea na ndugu yake alijibu

“Msiniulize mimi, mwambieni yeye, sina shida. Akipiga sawa tutaongea. Ugomvi wetu umevunja ukaribu mkubwa katika familia”

“Nilishasamehe na nipo sawa sina tatizo nae tena. Wakati wa tukio lile alikuwa Hispania. Alipordui tuliongea kidogo.”

“Alinieleza kila kitu. Nilimwelewa juu kwa juu kwa sababu baadhi ya mambo hakupenda kuyaongelea kiundan” Rodri

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here