Home Kimataifa Sir Ole Gunnar ataipeleka United nafasi ya 4 leo?

Sir Ole Gunnar ataipeleka United nafasi ya 4 leo?

3683
0

Fulham vs Manchester United, mchezo huu utapigwa katika dimba la Craven Cottage, majira ya saa 15:30 jioni.

Fulham, wameshinda michezo mitatu kati ya michezo 27 ya ligi kuu England dhidi ya Manchester United, sare mara 3 na amepoteza mara 19 pia kwenye michezo miwili ambaye Fulham, alimfunga Manchester United, katika uwanja wake wa nyumbani ilikuwa mwaka 2009.

Manchester United, hajapoteza mchezo hata moja kati ya michezo 10 ya ligi kuu England dhidi ya Fulham, ameshinda mara 8 na sare mara 2.

Fulham, wamepoteza michezo 20 dhidi ya Arsenal, kwenye ligi kuu na kama Manchester United, atashinda basi atakuwa na yeye amemfunga Fulham, michezo 20.

Fulham, wameshinda michezo miwili kati ya michezo mitatu ya mwisho kwenye uwanja wa nyumbani katika ligi kuu England, na amepoteza mara 1.

Manchester United, hawajapoteza mchezo hata moja kati ya michezo 8 ya ligi kuu England chini ya Ole Gunnar, ameshinda michezo 7 na sare mara 1wamefunga mabao 20 na kuruhusu mabao sita.

Manchester United, wanaangalia uwezekano wa kushinda mchezo wa sita mfululizo katika uwanja wa ugenini kwenye michuano yote mara ya mwisho ilikuwa May 2009.

Fulham, wamepoteza michezo 22 kati ya michezo 23 ya ligi kuu England dhidi ya timu sita kubwa za juu na sare mara 1 mara ya mwisho alimfunga Tottenham kwa bao 1-0 March mwaka 2013 wamefungwa mabao 25 na kufunga mabao 5.

Asilmia 80 ya mabao ya mshambuliaji wa klabu ya Fulham, Aleksandor Mitrovic, kwenye ligi kuu msimu huu amefunga katika uwanja wa nyumbani.

Claudio Ranier, amepata ushindi michezo miwili kati ya michezo 13 ya ligi kuu dhidi ya Manchester United, ushindi mara 2 sare mara 2 na kupoteza mara 5.

By Azizi _Mtambo 15

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here